Nav bar

Jumatano, 7 Desemba 2022

DKT. TAMATAMAH AFANYA MAZUNGUMZO NA WATAALAM KUTOKA GIZ - EMPLOYMENT AND SKILLS DEVELOPMENT IN AFRICA (E4D)

 


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah akiwa kwenye  picha ya pamoja na wataalam  kutoka GIZ- Employment and Skills Development in Africa (E4D), Dkt Francis Mwaijande( wa kwanza kushoto) na Dkt. Cris Horrill (wa pili kushoto) mara baada ya kikao kifupi cha kujadiliana kuhusu utafiti wa kubaini mahitaji ya ajira na ujuzi yaliyopo kwenye Sekta hiyo ili kuendana  na dhana ya Uchumi wa Buluu, kilichofanyika kwenye Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma (29.11.2022).


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mradi wa USAID - Lishe Endelevu kutoka Shirika la Save the Children Dkt. Joyce Kaganda(wa tatu kutoka kushoto) mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ofisi za mtumba kilicholenga  kupata mrejesho wa utekelezaji wa Mradi huo na kubainisha mipango ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Taasisi hiyo na Sekta ya Uvuvi ili kuongeza upatikanaji wa samaki na kuboresha Lishe. Wengine katika picha ni Watendaji wa Mradi wa USAID Lishe Endelevu  na Wataalam wa Sekta ya Uvuvi. (29.11.2022) Mkoani Dodoma.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni