Nav bar

Jumatano, 2 Novemba 2022


 Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akihutubia wananchi wa Kijiji cha Kibengu, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wakati wa ziara ya mawaziri wa kisekta ya  kutatua migogoro ya ardhi kwa Vijiji 975 nchini,  Oktoba 26,2022 Mkoani Iringa.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (wa pili kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya makazi Dkt. Angelina Mabula ( katikati), Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego (wa pili kutoka kulia)  na viongozi wengine mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa  Iringa za kutatua changamoto za migogoro ya ardhi, Oktoba 26,2022.

Sehemu ya wananchi waliohudhiria Mkutano wa hadhara wa Mawaziri wa Kisekta wanaoshughulikia kutatua migogoro ya ardhi kwenye Kijiji cha Kibengu, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Oktoba 26,2022.

Mhe. Abdallah Ulega (Mb.), Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi akihutubia wananchi wa Kitongoji cha Luduga kilichopo Kijiji cha Mpanga, Wilaya ya Wanging'ombe - Njombe. Hii ni katika ziara ya Mawaziri wa Kisekta kutatua migogoro ya ardhi ya Vijiji 975 nchini (27.10.2022).

Sehemu ya wananchi wa Kitongoji cha Luduga kilichopo Kijiji cha Mpanga, Wilaya ya Wanging'ombe - Njombe wakimsikiliza Mhe. Abdallah Ulega (Mb.), Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi. Katika Hotuba yake, aliwaeleza fursa kubwa waliyonayo ikiwa watafuga ng'ombe wa maziwa. Hii ni kwa kuwa hali ya hewa ya maeneo haya ni nzuri, chakula kipo cha kutosha na soko la zao hilo lipo jirani kwa uwepo wa Viwanda hususan Kiwanda kikubwa cha ASAS Mkoa jirani wa Iringa. Aidha, alitoa wito waanzishe pia vyama vya Ushirika vya Maziwa kama walivyofanya kwa mazao mengine. Walioketi meza kuu ni Viongozi wakiongozwa na Mhe. Dkt. Angeline Mabula (Mb.), Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Kisekta na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi (27.10.2022).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni