Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ugani wa Uvuvi na Ukuzaji viumbe maji Bw. Anthony Dadu akieleza fursa zinazotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa wavuvi ikiwa ni pamoja na kukopeshwa boti na vizimba bila riba wakati wa mafunzo yaliyofanyika kwenye mwalo wa Nyamkazi Mkoani Kagera Novemba 18,2022
Afisa Uvuvi Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Bw. Clemence Katunzi akitoa elimu kwa wavuvi juu ya madhara ya nyavu haramu ambazo wavuvi wengi hupenda kutumia na hivyo watumie nyavu sahihi na zitakazowasaidia kuvua kwa amani na kuondokana na migogoro kwenye mwalo wa Nyamkazi Mkoani Kagera, Novemba 18,2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni