WAKALA ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) wamesaini mkataba wa ushirikiano na Chuo cha Shandong nchini China ikiwemo kujenga chuo cha mifugo mkoani Songwe.
Pia watakuwa wakibadilishana mitaala,wanafunzi na wakufunzi lengo likiwa ni kuongeza ubora wa wataalamu katika sekta ya mifugo.
Akizungumza leo Novemba 18,2022 Jijini Dodoma Wakati wa kusaini mkataba huo uliofanyika kwa njia ya Mtandao,Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk Charles Mhina amesema ushirikiano huo utalenga katika baadhi ya maeneo.
Ameyataja maeneo hayo ni kwa wanafunzi wanaosoma Sayansi ya Mifugo na masomo mengine ya Udaktari wa mifugo na ufugaji wa viumbe maji.
“Pia walikubaliana pia wawe wanabadilishana mitaala na namna gani ya kuweza kuwanufaisha,”amesema Dk.Mhina
Aidha Dkt.Mhina amesema katika mahusiano hayo ambayo tayari wameyaanza tangu mwaka 2021 walikubalina na walikuwa na rasimu ya mkataba kwamba waanzishe kituo cha mafunzo ndani ya Rita.
Amesema mara baada ya kusaini nyaraka hizo sasa wamefungua rasmi uanzishwaji wa kituo hicho ambacho kitakuwa ni cha kisasa.
Pia ushirikiano unaelenga kuboresha mahusiano katika utekelezaji kuna maeneo yatahuisika ikiwemo kuijengea uwezo Taasisi ya Lita pamoja na kuboresha ufundishaji katika matawi yote pamoja na kuongeza uwezo wa walimu kutoa mafunzo.
Amesema wanaanza utekelezaji na tunamengi ya kujifunza kutoka kwa wachina
“Tunadhani kwa ushirikiano huu utafungua wigo wa kushirikiana zaidi na kuboresha baada ya hili tunaamini na taasisi zetu zingine nazo zitajifunza,”amesema Dk Mhina.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo Lita,Dk Pius Mwambene amesema mkataba huo unalenga kuanzisha kampasi ya 9 na wamepata eneo Mbozi Mkoani Songwe
Amesema wamenza mazungumzo ya chuo hicho mwaka 2019 kwa msaada mkubwa wa balozi wa Tanzania nchini India Mberwa Kairuki.
“Alijaribu kutuunganisha hasa katika sekta kuu ya kilimo bahati nzuri tuliwapata na mwaka 2021 tulisaini makubaliano katika kutoa mafunzo,”amesema Dkt.Mwambene
Dkt.Mwambene,amesema mafunzo wanayotoa ni ya kuwatengeneza vijana wataalamu wa mifugo ambao wanaenda kuwa wahudumu katika ngazi ya kijiji kata na wilaya kama maafisa mifugo wasaidizi.
Amesema baada ya kuanzisha mahusiano hayo wameendelea kuangalia maeneo ambayo wanaanza nayo na wamekubaliana kuanzisha chuo hicho.
Amesema wamendaa mkataba wa kujenga chuo hicho ndani ya miaka mitatu katika eneo la Songwe na kitafundisha vijana hao.
“Pia kitatumika kuwaandaa vijana ambao watakuwa tayari kwenda kusoma China kwa mwaka wa tatu hapa watasoma kwa miaka miwili halafu mwaka wa tatu wataenda kuumalizia nchini China,”amesema.
Amesema wakitoka huko wawe na elimu ya kutosha hivyo wanaishukuru Serikali ya Wachina na wanategemea kujenga chuo ambacho kitakuwa ni cha mfano.
KAIMU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk Charles Mhina akikata utepe kuashiria kusainiwa kwa mkataba wa ushirikiano na Chuo cha Shandong Cha nchini China na Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) hafla iliyofanyika kwa njia ya Mtandao leo Novemba 18,2022 jijini Dodoma.
KAIMU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk Charles Mhina akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) kuingia mkataba wa ushirikiano na Chuo cha Shandong Cha nchini China hafla iliyofanyika kwa njia ya Mtandao leo Novemba 18,2022 jijini Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni