Nav bar

Jumatano, 19 Oktoba 2022


 Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) ilipata Mwaliko kutoka Shirika la Afya ya Wanyama la Dunia (OIE) kushiriki warsha ambapo Dkt. Hamisi Nikuli (Mkurugenzi Msaidizi Ukuzaji Viumbe Maji – Bahari) Mwakilishi wa Shirika hilo hapa nchini na Bwana Longinus Tegulirwa (Afisa Uvuvi) waliiwakilisha Wizara katika Warsha iliyofanyika Maputo - Msumbiji tarehe 11- 13/10/2022. Nchi 22 zilishiriki warsha hiyo. Lengo la warsha hii ni kujadili namna ya kupunguza matumizi ya madawa katika ufugaji samaki ili kuepusha madhara kwa walaji wa samaki kwa kuboresha mbinu za uzalishaji, udhibiti wa magonjwa na kusimamia ustawi wa viumbe maji.

Dkt Hamisi Nikuli (Kulia) akitoa mada kwa washiriki juu ya ukubwa wa madhara duniani ya matumizi ya madawa yasiyofuata Sheria, Kanuni na miongozo kwa walaji na afya ya viumbe maji ikijumuisha kuwepo kwa mabaki ya madawa katika minofu ya samaki yanayoweza kuathiri afya ya walaji na kuwepo kwa usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya madawa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni