Nav bar

Jumapili, 23 Oktoba 2022

WIZARA YAWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI INAYOTEKELEZWA KUPITIA MKOPO WA DIRISHA LA EXTENDED CREDIT FACILITY LA SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI (IMF)

 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (wa pili kutoka kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo (wa pili kutoka kulia) Taarifa ya Miradi inayotekelezwa kupitia mkopo wa dirisha la Extended Credit Facility la Shirika la Fedha Duniani (IMF) wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu anayesimamia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Mifugo, Dkt. Charles Mhina (17.10.2022)


Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya Bajeti pamoja na viongozi na wataalam wa Wizara wakifuatilia mawasilisho ya taarifa za Miradi inayotekelezwa kupitia mkopo wa dirisha la Extended Credit Facility la Shirika la Fedha Duniani (IMF) wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika bungeni Jijini Dodoma. (17.10.2022)


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (wa tatu kutoka kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi na wataalam wa Wizara mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kilichofanyika bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu anayesimamia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah. (17.10.2022)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni