Nav bar

Jumapili, 23 Oktoba 2022

WATAALAM WAFANYA TATHMINI YA WANUFAIKA WA MIKOPO YA BOTI NA MWANI

Afisa Mifugo mkoa wa Katavi Bw. Zidihery Mhando akiwatambulisha watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kutoka Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Tanganyika Bw. Philemon Mwita (katikati) walipifika kwenye Wilaya ya hiyo kwa lengo la kufanya tathmini ya maombi ya mikopo ya boti kwa wanavikundi na wanachama wanaojihusisha na shughuli za Uvuvi kwenye mkoa wa Katavi Oktoba 17,2022

Afisa Uvuvi Wilaya ya Tanganyika Bw. Dismas Kessy akifungua kikao cha kufanya tathmini ya maombi ya mikopo ya vikundi, makampuni, vyama vya ushirika na watu binafsi wanaojihusisha na shughuli za Uvuvi inayotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kilichofanyika  kwenye wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Oktoba 17,2022.

Afisa biashara Mwandamizi kutoka Dawati la Sekta binafsi chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Eliakim Mniko  akitoa maelezo ya mkopo wa boti za kisasa za uvuvi kwa vyama ,vikundi,makampuni na watu binafsi (hawapo pichani) wanaojihusisha na Uvuvi katika ukanda wa Ziwa Tanganyika ili kuwawezesha kufanya Uvuvi endelevu wenye tija utaowasaidia  kujiongezea kipato na kupunguza umaskini, kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Oktoba 17,2022.

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Emmanuel Shekolowa (wa tatu kutoka kushoto) akielezea bei ya boti na ubora wake kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Bw.Philemon Mwita (Katikati) wakati wa ziara Yao Mkoani humo, Octoba 17, 2022.

Afisa biashara kutoka Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Bw. Patrick Kapungu akitoa elimu ya mkopo na ukomo wa madeni kwa wanavikundi na wanachama wa Wilaya ya Tanganyika (hawapo pichani) wanaojihusisha na shughuli za Uvuvi Mkoani Katavi, Oktoba 17,2022.

Viongozi wa vikundi na vyama vya ushirika wakisikiliza kwa makini maelezo ya bei na ubora wa boti yaliyokuwa yakitolewa na afisa Uvuvi mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na na Bw. Emmanuel Shekolowa (hayupo pichani) wakati wa kikao kifupi kilichofanyika kwenye wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Oktoba 17,2022

Watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakipitia taarifa za vyama vinavyojihusisha na shughuli za uvuvi na kuona kama zimekamilika na kukidhi vigezo vya kupata mkopo wa boti za uvuvi zitazoenda kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku za uvuvi . Oktoba 17, 2022 kwenye Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi.

Afisa biashara mkuu kutoka dawati la sekta binafsi  chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Eliakim Mniko (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya viongozi wa vyama vya ushirika na vikundi vinavyojishughulisha na shughuli za  Uvuvi mara baada ya kufanya tathmini ya maombi ya mikopo ya boti za Uvuvi  zinazotarajiwa kutokewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Benki ya maendeleo ya  kilimo Tanzania (TADB) kama yamekidhi vigezo vya kupata mkopo huo kwenye wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi. Oktoba 17,2022.

Mkurugenzi Msaidizi Ukuzaji Viumbe Maji Bahari, Dkt.Hamis Nikuli ( kulia ), meza kuu,  Mkurugenzi wa Msaidizi wa Ugani na Ukuzaji Viumbe Maji  Bw.Antony Dadu ( kushoto ) wakiwa  kwenye kikao cha kuhakiki fomu za maombi ya Mikopo ya Mradi wa Uvuvi wa Boti, na Kilimo cha Mwani toka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Lengo la kikao hicho katika  Halmashauri ya Bagamoyo ni  kukagua na kuhakiki fomu za maombi ya mikopo ya wavuvi kama zimejazwa sawasawa au kuna malekezo ya ziada yanayohitajika katika ujazaji wa fomu hizo kikamilifu ili Banki ya Maendeleo ya Kilimo iweze kutoa mikopo hiyo kwa waombaji waliotimiza vigezo vya Mkopo. Mikopo hiyo isiyokuwa na riba inatolewa kwa waombaji wanaotimiza masharti na vigezo ikiwemo waombaji kuwa katika Vikundi vya Uvuvi vilivyosajiliwa,Ushirika wa Wavuvi,Wavuvi binafsi wanajidhamini kupita mali zao wanazomiliki,na Makampuni ya Uvuvi wanajidhamini kupitia mali za makampuni yao.Kikao kimefanyika katika Hamashauri ya Bagamoyo. (17.10.2022)

Mkurugenzi msaidizi Idara ya Ukuzaji Viumbe maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Imani Kapinga akiongea na vikundi, wanachama, makampuni na watu binafsi wanaojihusisha na shughuli ya Uvuvi wakati wa ziara yao kwenye Halmashauri ya  Wilaya ya Musoma Mkoani Mara ya kufanya tathmini ya kuona kama wamekidhi vigezo vya maombi ya mkopo wa maboti na vizimba vinavyotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Mkoani hapo Oktoba 18, 2022

Afisa Biashara kutoka benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Bw. Marko Samson (kushoto) akitoa maelezo ya vigezo vinavyoitajika kwa vikundi, vyama vya ushirika , makampuni na watu binafsi wanaojihusisha na shughuli za uvuvi   kupata mkopo wa vizimba na maboti yanayotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB)  kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mkoani Mara, Oktoba 18, 2022.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi kanda ya Mwanza (TAFIRI),  Dkt. Baraka Sekadende akitoa maelezo juu ya upatikanaji wa kibali cha ufugaji kwenye vizimba wakati akitoa elimu na kufanya tathmini ya maombi ya mkopo wa vizimba na maboti yanayotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania TADB kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mkoani Mara. Oktoba 18,2022

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Imani Kapinga (wa pili kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Afisa Biashara kutoka benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Bi. Eveline Shayo (wa kwanza kulia), Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Mkomanile Mahundi (wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Dkt. Baraka Sekadende (wa kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya  Musoma Mkoani Mara, Oktoba 18,2022.

Timu ya wataalam toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Benki ya Maendeleo ya Kilimo    ( TADB ), na Dawati la Sekta Binafsi, ikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Ugani wa uvuvi na Huduma za Ukuzaji Viumbe Maji,Bw.Antony Dadu aliyesimama , akiongea na  Wadau wa Uvuvi, wanaomba Mikopo ya Boti,vifaa vya kilimo cha Mwani kwa upande wa Pwani wa Bahari ya Hindi,ambapo shughuli za uvuvi na kilimo cha mwani vina tekelezwa kwa kiwango kikubwa.Hivyo ili kuwa na uvuvi na kilimo cha mwani chenye tija endelevu mikopo ya Boti na Vifaa vya mwani              inatolewa  na Wizara kupitia Mradi wa Boti,Vizimba na Kilimo cha mwani.Timu ya wataalam leo inaongea na wadau hao  na hatimaye kuhakiki fomu za  mikopo hiyo katika soko la samaki la  Feri Jijini Dar es Salaam (19.10.2022).

Timu ya uhakiki wa mikopo kwa Wadau wa Uvuvi inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Benki ya Wakulima TADB ikiongozwa na Afisa Uvuvi Mwandamizi Dkt. Ambakisye Simtoe (wa kwanza kushoto ) ikiwa ofisini kwà Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bw. Majid Myao (meza kuu) ikijitambulisha  na lengo la ziara yao Mkoani hapo kuwa  ni kuonana na vikundi ,vyama vya ushirika, wavuvi binafsi  na Makampuni ya  Uvuvi yaliyomba mikopo ya  Mradi wa Boti  Vizimba na Kilimo cha Mwani  ili wahakiki fomu za maombi ya mkopo huo na kutoa maelekezo ya ufafanuzi pale ambapo hapajaeleweka kwa wadau hao.Kikao kilifanyika katika ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Lindi. (19.10.2022)

Wataalam toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiongozwa na Wakurugenzi wasaidizi, Ukuzaji viumbe Maji Bahari Dkt.Hamisi Nikuli (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Ugani wa Uvuvi, na Ukuzaji Viumbe Bw. Antony Dadu wa  kwanza (wa kwanza kushoto) wakiwa ofisini kwa Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bi Zuena Omari (katikati)  kwa ajili ya kujitambulisha na kuelezea lengo la ziara yao Mkoani ambalo ni Kufuatilia na kuhakiki fomu za maombi ya mikopo inayotolewa na Wizara ya  Mifugo na Uvuvi kwa Wadau wa Uvuvi wanaokopeshwa Boti,Vifaa ufugaji samaki katika   Vizimba, na Vifaa vya Kilimo cha Mwani,mkopo huu hauna riba,mkopo ni wa miaka mitano ila mkopaji anapewa mwaka mmoja upite ndipo anaanza kurudisha kwa miaka  minne.(17.10.2022)

Afisa biashara Mwandamizi kutoka Dawati la Sekta binafsi chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Eliakim Mniko (katikati)  akielezea lengo la ziara yao kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Esther Mahawe ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya taarifa za  vyama ,vikundi,makampuni na watu binafsi wanaojihusisha na Uvuvi na kuona kama wanakidhi vigezo vya kupata mkopo wa vifaa vya Uvuvi ili kuwawezesha kufanya Uvuvi endelevu wenye tija utaowasaidia  kujiongezea kipato na kupunguza umaskini, Mkoani Kigoma Oktoba 20,2022.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Bi. Esther Mahawe akiishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kwa kuleta fursa ya mkopo wa maboti Mkoani Kigoma kwani itaenda kuwanufaisha  wavuvi  kwa kuvua kisasa na kwa tija hivyo kuongeza kipato cha mvuvi mmoja mmoja na jamii kwa  ujumla , Oktoba 20,2022.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Bi. Esther Mahawe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na afisa biashara kutoka Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB), mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika ofisini kwake chenye lengo la kufanya tathmini ya maombi ya mikopo ya boti za kisasa za Uvuvi  zinazotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) na kuona kama wamekidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo kilichofanyika ofisini kwake wilayani hapo Mkoani Kigoma, Oktoba 20,2022.

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Emmanuel Shekolowa  akieleza bei ya boti na ubora wake kwa wanachama, wanavikundi, makampuni na watu binafsi wanaojihusisha na shughuli za Uvuvi  Mkoani Kigoma, Octoba 20, 2022.

Afisa biashara kutoka Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Bw. Patrick Kapungu akitoa elimu ya mkopo na ukomo wa madeni kwa wanavikundi na wanachama  wanaojihusisha na shughuli za Uvuvi Mkoani Kigoma, Oktoba 20,2022.

Picha ya Pamoja ya Timu ya Wataalam toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiongozwa na Wakurugenzi wasaidizi  wa Ukuzaji Viumbe Maji Bahari  Dkt. Hamisi Nikuli watatu toka (kuli ), wa pili ni Mkurugenzi Masidizi wa Ugani wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji Bw.Antony Dadu wa  pili toka (kulia), Bw.Augustine Mshanga Mchumi, wa kwanza (kulia) toka Dawati la Sekta Binafsi,Mtaalam wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ( TADB ) Bw.Richard Sempindu wa pili   toka ( kushoto ) na  katikati ni Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni Bw.James Mkumbo picha imechukuliwa ofisi ya Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni, lengo la ziara ya wataalam katika ofisi hiyo ni kujitambulisha kuwa wamekuja kwa kazi ya kuhakiki fomu za mikopo ya wadau wa uvuvi wanao kopeshwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Boti, na Vizimba (20.10.2022).

Watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiwa kwenye ofisi ya kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ukerewe Bw. Goodluck Mtigandi (katikati) wakati wa ziara yao kwenye Halmashauri hiyo yenye lengo la kufanya tathmini ya maombi ya mkopo wa vizimba na maboti kwa makampuni, vikundi, vyama vya ushirika na watu binafsi yanayotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB)  na kuona kama wamekidhi vigezo vya kupata mkopo Huo, Oktoba 21,2022

Afisa Mfawidhi Bw. Elinsa Massawe akitoa maelezo ya kina juu ya mikopo ya boti na vizimba inayotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kwa vikundi, vyama vya ushirika, makampuni na watu binafsi  waliopo katika Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Oktoba 21,2022

Wanawake toka eneo la Buyuni Manispaa ya Kigamboni wanao jishughulisha na Kilimo cha Mwani  Wilaya ya Kigamboni wakimsikiliza kwa Makini Mkurugenzi Msaidizi Ukuzaji viumbe maji Bahari,Dkt.Hamisi Nikuli wa kwanza (kushoto) meza kuu,ambapo amewaleza Wakulima hao wa Mwani kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatoa Mikopo ya kwa Kilimo cha  Mwani kupitia Mradi wa Boti, Kilimo cha Mwani na Ufugaji wa samaki katika Vizimba,hivyo timu ya Wataalam toka Wizarani tuko hapa kwa lengo la kuhakiki na kutoa Ufafanu wa fomu za mkopo wa Mwani  kwa wanawake wa kata hii ya Buyuni Wilaya ya Kigamboni leo (21.10.2022)

Mkuu wa Dawati la Sekta Binafsi Bw.Ambakisye Mtoe aliyesimama mbele mwenye  (shati la bluu), akiongea na wadau wa Uvuvi wanaomba mikopo ya Maboti na Vifaa vya Kilimo cha Mwani katika Hamashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi. Timu ya Wataalam wa Uvuvi toka Dodoma imefanya ziara ya kuwatembelea wadau wa Uvuvi kwa Lengo la kuhamasisha na kuhakiki fomu za maombi ya mikopo ya Mradi wa Boti na Vifaa vya Kilimo cha Mwani kwa upande wa eneo la ukanda wa Bahari ya Hindi inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB ), kwa upande wao wavuvi hao wamekuwa na ushauri wa mikopo inayotolewa kwa upande wa Boti za Fibre,walitoa maoni kuwa wanataka,  Boti zilizoundwa kwa  mbao kwa kuwa ni imara na zinahimili mawimbi ya bahari kuliko za Fibre siyo imara sana zinapigwa na mawimbi, hivyo ushauri wao ulipokelewa na wataalam utafikishwa ngazi za juu watapewa mrejesho.(18.10.2022).

Timu ya wataalam wa Uvuvi toka Wizarani Dodoma, Banki ya Mwendeleo ya Kilimo,(TADB ) ikiongozwa na Mratibu wa Dawati la Sekta Binafsi ya Uvuvi Dkt.Ambakisye Mtoe wa pili ( kulia) wakijitambulisha kwa Mkurugenzi Mtendaji ,w Bw.Kassim Ndumbo ( meza kuu ) Halmashauri ya Mafia,ambapo amemweleza Lengo la ziara yao ni kukutana na wadau wa Uvuvi ambao wako katika Vikundi, Ushirika,Watu Binafsi na Kampuni za Uvuvi ili kuhakiki na kutoa maelekezo ya kuhamasisha wadau hao kukopo Boti za Kisasa na Vifaa vya kilimo cha Mwani vinavyokopeshwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Maboti na Vizimba na Mwani na kuratibiwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ( TADB ).ambapo wavuvi wakipata mikopo hii  wataboresha shughuli zao kuwa na tija endelevu. (24.10.2022)

Afisa uvuvi Manispaa ya Ilemela Bw. Ivon Maha akikabidhi   maombi yaliyokamilika ya mikopo ya boti za uvuvi na vizimba kwa  kiongozi wa msafara kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wa timu ya mikopo ya boti kwa Mkoa wa Mwanza, Simiyu na Mara Bi. Flora Luhanga (kulia) kwenye ofisi ya uvuvi iliopo Soko la Kimataifa la Samaki Kirumba Jijini Mwanza, Oktoba 26,2022.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni