Afisa Mifugo msaidizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Rehema Kombe (kulia) akimpa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema,maelezo ya ukuaji wa mbegu ya malisho aina ya Juncao muda mfupi leo (12.10.2022) baada ya Mhe. Mjema kufika kwenye banda la Wizara hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Halmashauri ya Mji, Bariadi mkoani Simiyu yanakofanyika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani.
Daktari Utafiti wa Mifugo Mwandamizi kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari nchini (TVLA) kanda ya Ziwa Mashariki Dkt. Raphael Paulo (kushoto) akimueleza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema matumizi ya chanjo ya ugonjwa wa mdondo muda mfupi leo (12.10.2022) baada ya Mhe. Mjema kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Halmashauri ya Mji, Bariadi mkoani Simiyu yanakofanyika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani.
Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo nchini (TALIRI) kituo cha Kongwa, Bw. Jefta Rwegasira (kushoto) akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (mwenye miwani), mchoro unaoonesha hatua za uhimilishaji wa kuku muda mfupi leo (12.10.2022) baada ya Mhe. Mjema kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Halmashauri ya Mji, Bariadi mkoani Simiyu yanakofanyika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kulia) akipata maelezo ya namna Bodi ya Maziwa nchini (TDB) inavyotekeleza majukumu yake kutoka kwa Mteknolojia wa Chakula wa Bodi hiyo Bi. Deorinidei Mng'ong'o (kushoto) muda mfupi leo (12.10.2022) baada ya Mhe. Mjema kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Halmashauri ya Mji, Bariadi mkoani Simiyu yanakofanyika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani.
Mteknolojia wa Chakula kutoka Bodi ya Maziwa nchini (TDB) Bi. Deorinidei Mng'ong'o (kulia) akimkabidhi zawadi ya Maziwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema muda mfupi leo (12.10.2022) baada ya Mhe. Mjema kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Halmashauri ya Mji, Bariadi mkoani Simiyu yanakofanyika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani.
Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Kitengo cha Uthibiti Ubora na Usalama wa Mazao ya Uvuvi kanda ya Ziwa Victoria Bw. Prosper Mremi (kushoto) akimueleza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kulia) faida za mabondo (aliyoyashika) muda mfupi leo (12.10.2022) baada ya Mhe. Mjema kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Halmashauri ya Mji, Bariadi mkoani Simiyu yanakofanyika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani.
Mmoja wa wadau wa sekta ya Uvuvi waliopo kwenye Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Sylvia Doto (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema zawadi ya dagaa wa Ziwa Victoria waliokaushwa kwa jua muda mfupi leo (12.10.2022) baada ya Mhe. Mjema kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Halmashauri ya Mji, Bariadi mkoani Simiyu yanakofanyika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni