WAWEKEZAJI KUTOKA ISRAEL WAWASILISHA TEKNOLOJIA MPYA KWENYE UVUVI WA BAHARI KUU.
Wawekezaji kutoka Nchi ya Israel wa kampuni SVIVA SWISS AG wamewasilisha Teknolojia mpya inayotumiwa katika kulinda rasilimali za uvuvi kwenye ukanda wa Bahari kuu kwenye kikao kilichofanyika kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi upande wa sekta ya uvuvi na Wawekezaji hao. Jijini Dodoma, 12 Oktoba 2022.
Katibu wa Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah amesema wawekezaji hao wamewasilisha teknolojia ambayo inatumiwa katika ulinzi wa rasilimali za uvuvi katika maeneo makubwa kama ya maziwa na maeneo ya ukanda maalaum wa uchumi wa bahari kuu.
Dkt. Tamatamah amesema wawekezaji wametoa takwimu ya mwaka mmoja ya kuanzia mwezi Agosti 2020 hadi Agosti 2021 na wakatoa idadi ya meli ambazo zinavua kwa uvuvi haramu na hazikuandikishwa.
"Kwahiyo kikao hichi tulichoamua wataalamu wa Israel wataondoka na wataalamu wa Mamlaka ya kusimamia Uvuvi wa Bahari kuu Zanzibar ili waende kuwaonyesha jumba letu kule Zanzibar kwenye chumba cha mitambo ili wafanye uchambuzi wa kile wanachokisema na kile ambacho sisi tunakifanya" Amesema Dkt. Tamatamah.
Dkt. Tamatamah ameongezea kwa kusema, baada ya wawekezaji hao kutembelea na kufanya kikao huko Zanzibar, kama kutakuwa na gap ya taarifa ya hao wawekezaji na system tunayoitumia Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu Zanzibar wataishauri wizara ya Mifugo na Uvuvi kama kuna umuhimu wa kuchukua teknolojia ya wawekezaji hao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na sekta ya uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah (watatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawekezaji kutoka Nchi ya Israel(kushoto) na wataalamu wa sekta ya uvuvi mara baada ya kumaliza kikao cha kupitia mawasilisho ya wawekezaji hao kilichofanyika Jijini Dodoma,Tarehe 12 Oktoba 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni