Afisa biashara Mwandamizi kutoka Dawati la Sekta binafsi chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Eliakim Mniko akitoa maelezo ya mkopo wa boti za kisasa za uvuvi kwa vyama ,vikundi,makampuni na watu binafsi wanaojihusisha na Uvuvi ili kuwawezesha kufanya Uvuvi endelevu wenye tija utaowasaidia kujiongezea kipato na kupunguza umaskini, kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa Oktoba 12, 2022.
Afisa Biashara kutoka benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB), Bw. Patrick Kapungu akitoa maelezo ya namna maandiko ya biashara yanavyotakiwa kuandikwa kwa vyama, vikundi, watu binafsi na makampuni yanayojiusisha na shughuli za uvuvi wakati wa kikao kifupi kilichofanyika kwenye Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa Oktoba 12,2022.
Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, Bw. Emmanuel Shekolowa (wa tatu kutoka kulia) akichangia hoja wakati wa kikao kifupi cha kufanya tathmini ya maombi ya mkopo wa boti za uvuvi zinazotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kilichofanyika kwenye Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa Oktoba 12,2022.
Afisa biashara Mwandamizi kutoka Dawati la Sekta binafsi chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Eliakim Mniko (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wavuvi, maafisa Uvuvi na Afisa kutoka benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB) mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika kwenye Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, lengo likiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya wanufaika wa mikopo isiyo na riba ya boti za kisasa za Uvuvi zinazotarajiwa kutolewa na Wizara hiyo kupitia Benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) na kuona kama wamekidhi vigezo Ili waweze kukopesheka na kupata boti zitakazowasaidia wavuvi kufanya Uvuvi endelevu wenye tija utaowasaidia kujiongezea kipato na kupunguza umaskini, Oktoba 12,2022.
Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Clemence Katunzi akitoa elimu ya mkopo wa boti za kisasa za uvuvi na faida zake kwa vyama ,vikundi,makampuni na watu binafsi wanaojihusisha na Uvuvi ili kuwawezesha kufanya Uvuvi endelevu wenye tija utaowasaidia kujiongezea kipato na kupunguza umaskini, kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza , Oktoba 12, 2022.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Bi. Mary Mwangisa (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji kutoka kwenye Wizara hiyo Sekta ya Uvuvi na Katibu wa Mbuge Jimbo la Buchosa Bw. Julius Butogwa, nje ya Ofisi ya Mbuge wa Jimbo hilo kabla ya kuanza mafunzo na kufanya tathmini kwa wanufaika wa mikopo isiyo na riba ya boti za kisasa za Uvuvi na vizimba zinazotarajiwa kutolewa na Wizara hiyo kupitia Benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) na kuona kama wamekidhi vigezo vya maombi ya mkopo wa vizimba na maboti hayo kwenye Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza Oktoba 12, 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni