Nav bar

Jumatano, 19 Oktoba 2022

 


Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA - Tanga) Dkt. Oliver Manangwa (kushoto) akizungumza na wanamichezo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo Oktoba 12,2022 walipotembelea Ofisi za Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Mkoani Tanga kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo.


Wanamichezo wa timu za Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya mapango ya Amboni yaliyopo Jijini Tanga walipofanya utalii wa ndani kwenye mapango hayo leo Oktoba 12,2022.


Mkuu wa Kituo cha TALIRI (Tanga) Dkt. Zabron Nziku akitoa maelezo kwa ufupi kwa wanamichezo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo Oktoba 12,2022 kuhusu Taasisi hiyo ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) inavyofanya kazi, walipotembelea Ofisi za Taliri Tanga, kushoto kwa Dkt. Zabron Nziku ni Mwenyekiti wa Michezo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Ally Suru.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni