Mfugaji wa Samaki kwenye Mabwawa, Bw. Kayuni, akiwaelezea wataalamu wa uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Halmshauri ya Jiji la Dodoma, jinsi anavyoendesha ufugaji huo kwenye mabwawa na changamoto anazozipata kwenye ufugaji, wakati wataalamu hao walipomtembelea(06.09.2022) kwenye shamba lake lililopo kata ya Miyuji, Jijini Dodoma, Lengo ni kupokea changamoto wanazokutana nazo wafugaji na kutoa elimu ya namna bora ya ufugaji samaki kwenye mabwawa
Mkurugenzi wa taasisi ya Young World feeders Farms, Bw. Ray Peter, (wa pili kushoto) akiwaelezea wataalamu kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi, jinsi taasisi hiyo inavyoendesha ufugaji huo wa samaki kwenye mabwawa, walipoenda kutembelea wataalamu hao kwenye shamba hilo ili kujua changamoto wanazokutana nazo na kuwapa elimu zaidi juu ya ufugaji huo wa samaki, leo 06.09.2022. Dodoma.
Wataalamu wa ufugaji samaki kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Halmshauri ya Jiji la Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa taasisi ya Young World Feeders Farms Bw. Ray Peter ( wapili kushoto) walipoenda kutembelea shamba la ufugaji samaki kwenye mabwawa na kutoa elimu ya namna bora ya ufugaji samaki. 06.09.2022.
Mfugaji wa Samaki Dkt. Joseph Komba (watatu kulia) akiwaelezea wataalamu wa ufugaji samaki kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi namna anavyofuga na changamoto anazokumbana nazo kwenye ufugaji huo,, mara baada ya wataalamu hao walipoemda kumtembelea kwenye shamba lake lililopo Miyuji Jijini Dodoma.06.09.2022.
Muonekano wa bwawa la kufugia samaki lililozibwa na wavu kwa ajili ya kuzuia samaki wadogo kuliwa na ndege kwenye shamba la Dkt. Joseph Komba (hayupo pichani) lililopo Miyuji Jijini Dodoma, 06.09.2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni