Nav bar

Jumapili, 14 Agosti 2022

SIMBACHAWENE ATAKA WAFUGAJI KUWEKA HELENI MIFUGO

Na. Martha Mbena


Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera,uratibu na bunge  George Simbachawene amewataka Wafugaji kushiriki kwenye zoezi la kitaifa la uwekaji heleni za kieletriniki  katika mifugo .


Simbachawene ameyasema hayo wakati akifunga maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki ambayo yanafanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Manispaa ya Morogoro.


Amesema zoezi la uwekaji heleni ni zoezi la kitaifa hivyo Wafugaji wanawajibu wa kushirikiana na Serikali kwani linamanufaa makubwa kwao na Serikali .


Amesema Heleni hizo zitakua na uwezo wa kuunganishwa moja kwa moja na vifaa maalum na kudhibiti changamoto ya wizi kwani itakua inauwezo kuonesha mahali Mifugo ilipo.


Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene amewataka wataalam walioshiriki maonesho ya nanenane kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi ili kuinua kipato Chao kupitia sekta ya Mifugo,kilimo na Uvuvi.

Mgeni Rasmi wa sikukuu ya maadhimisho ya maonesho ya wakulima nanenane kanda ya Mashariki Morogoro, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. George Simbachawene, akipita kwenye mabanda mbalimbali ya maonesho hayo, (08.08.2022).


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni