Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Emanuela Mawoko (kushoto) akimpa mdau wa uvuvi elimu kuhusu madhara ya matumizi ya nyavu haramu ya kuvulia samaki (waliyoshika) mara baada ya mdau huyo kufika kwenye banda la Wizara hiyo lililopo kwenye Maonesho ya Nanenane kanda ya kati yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma (08.08.2022).
Afisa Mifugo Mwandamizi toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Idara ya DPMD) Ahmed Mziray (kulia) akipokea Kikombe cha Ushindi wa Kwanza kwa Taasisi za Serikali kwenye kilele cha kufunga Maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibi Tabora,Viwanja vya Ipuli toka kwa mgeni rasmi Mh.Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu wa jeshi la zima moto Thobias Andengenye (kushoto) (08.08.2022)
Picha ya pamoja ya washiriki wa Maonesho ya Wakulima Nanenane Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi ,2022 kanda ya Magharibi Mkoani Tabora wakiwa na kombe la Ushindi wa kwanza kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kwa Taasisi za serikali aliyeshikilia kombe hilo la ushindi ni meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dkt.Geofrey Mbata nje ya banda la Mifugo na Uvuvi Viwanja vya Ipuli Mkoani Tabora. (08.08.2022)
Mtaalamua wa utafiti wa wadudu aina ya Mbung'o Ndg. Ally Fussah (kulia) kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) akitoa elimu ya teknolojia ya kudhibiti Mbung'o kwa kutumia mitego na vitambaa vyenye dawa kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Wakala lililopo kwenye mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika kwenye uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya leo Tarehe 08/08/2022.
Muuzaji wa Vifaa vya Uvuvi kutoka Kampuni ya NYOTA VENTURE CO. LTD, Bw. Yahaya Makuhana, akimuelezea jinsi ya kutumia nyavu kwa upande wa baharini na Ziwani, Afisa Tawala Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Wamoja Ayubu, alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye siku ya kilele cha maonesho ya wakulima nanenane kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro. Agosti 08.2022.
Mchakataji na muuzaji samaki na dagaa kutoka ATUDI FISH SUPPLY, Bi Jane Mchopa, akimpatia maelekezo Afisa Tawala Mkuu, Bi Wamoja Ayubu, kuhusu namna bora ya kuchakata dagaa ili wasiwe na michanga kwa njia ya kukausha kwa moshi na chumvi, alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye siku ya kilele cha maadhimisho ya maonesho ya wakulima nanenane kanda ya Mashariki yaliyofanyika Mkoa wa Morogoro, Agosti 08,2022.
Afisa Tawala Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi sekta ya Mifugo, Bi Wamoja Ayubu, akisaini kitabu cha wageni (08.08.2022) muda mfupi baada ya kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye siku ya kilele cha maonesho ya wakulima nanenane kanda ya mashariki mkoani Morogoro.
Mfanyabiashara wa Maziwa kutoka kwa wasindikaji wa Maziwa wa Mbeya Milk, Bw. Joseph Adamson Kajange akitoa huduma ya Maziwa kwa Wananchi waliotembelea banda la Bodi ya Maziwa Tanzania ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wa unywaji Maziwa leo Agosti 8, 2022 kwenye kilele cha maonesho ya Kilimo (Nanenane) yaliyofanyika kitaifa Jijini Mbeya.
Mdau mpya wa Biashara ya Maziwa kutoka Mbezi kwa Msumi Jijini Dar Es Salaam, Bw. Geofrey Yambayamba (kushoto) akielekezwa jinsi ya kujisajili na kupata kibali cha Biashara ya Maziwa kwa njia ya mfumo kwa kutumia simu yake ya mkononi na Afisa Mteknolojia wa Chakula wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Bw. Kennedy Daniel katika banda la Bodi ya Maziwa Tanzania leo Agosti 8, 2022 kwenye kilele cha maonesho ya Kilimo (Nanenane) yaliyofanyika kitaifa Jijini Mbeya.
Afisa Mteknolojia wa Chakula wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Bw. Kennedy Daniel (kulia) akimpatia maelezo mwananchi aliyefika kupata msaada wa kitaalamu wa kuanzisha biashara ya jibini alipotembelea banda la Bodi ya Maziwa Tanzania leo Agosti 8, 2022 kwenye kilele cha maonesho ya Kilimo (Nanenane) yaliyofanyika kitaifa Jijini Mbeya.
Afisa Masoko kutoka Kampuni ya JEWJ ambao ni wadau wakubwa wa usambazaji na ufungaji wa mashine mbalimbali za kusindika Maziwa lakini pia washauri wa masuala mbalimbali kwenye Tasnia hiyo, Bw. William Mwangalabe akiwaelekeza Wananchi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Busekelo kazi zinazofanywa na Wadau hao wa Maziwa Nchini leo Agosti 8, 2022 katika Banda la Bodi ya Maziwa Tanzania kwenye kilele cha maonesho ya Kilimo (Nanenane) yaliyofanyika kitaifa Jijini Mbeya.
Wadau wa Tasnia ya Maziwa Jijini Mbeya wakipatiwa maelezo ya kina juu ya utambuzi wa ubora wa Maziwa na Afisa Mteknolojia wa Chakula wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Bw. Kennedy Daniel (kushoto) katika banda la Bodi ya Maziwa Tanzania leo Agosti 8, 2022 kwenye kilele cha maonesho ya Kilimo (Nanenane) yaliyofanyika kitaifa Jijini Mbeya.
Dkt. Qwari Bura (kulia) Meneja kituo cha Iringa pamoja na Dkt. Rajabu Mlekwa Meneja kituo cha Sumbawanga kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) wakiwa Mubashara leo tarehe 08/08/2022 kwenye kituo cha Radio cha Bomba FM kilichopo Mbeya mjini wakieleza kazi mbalimbali zinazofanywa na Wakala pamoja na Mipango mikakati iliyowekwa kuwafikia wafugaji wote nchini kuwapa elimu ya uchanjaji wa Mifugo yao, kuhakiki ubora wa vyakula vya Mifugo, kupima magonjwa ya mifugo pamoja na kuhakiki dawa za kuogeshea Mifugo.
Mtaalam wa ukuzaji viumbe maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Elisa Masawe (wa tatu kutoka kushoto) akitoa elimu ya kufuga samaki kwenye vizimba kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa kilele cha maonesho ya nanenane yaliyofanyika kwenye kiwanja cha Nyamhongolo Mkoani Mwanza Agosti 08, 2022.
Afisa Mfawidhi Kanda ya ziwa, Bw. Prosper Mremi (aliyesimama kulia) akieleza faida za mabondo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya nanenane yaliyofanyika kwenye kiwanja cha Nyamhongolo Mkoani Mwanza Agosti 08, 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni