Na. Edward Kondela
Serikali imesema ipo katika hatua muhimu za utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Mbari za Ng’ombe wa Maziwa nchini (ADGG) unaotekelezwa na Taasisi ya Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) ili mradi huo uwe na tija zaidi kwa wafugaji.
Akizungumza leo (05.08.2022) wakati akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa ng’ombe wa maziwa katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Mbeya, Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI Prof. Erick Komba amesema warsha hiyo ni muhimu katika kupima na kubaini maeneo ya maboresho wakati huu ambapo mradi unaingia awamu ya tatu.
Prof. Komba ameongeza kuwa warsha hiyo itasaidia kutolewa kwa maoni mbalimbali kutoka kwa wadau juu ya uboreshaji wa ukusanyaji wa takwimu, mfumo wa kupeleka mrejesho kwa wadau, mfumo wa taarifa za masoko ya mifugo na pembejeo zingine pamoja na kujadili maboresho ya utoaji huduma za uhimilishaji.
Aidha, ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika mradi wa ADGG hapa nchini kwenye awamu ya kwanza na pili kuwa ni kuanzishwa kwa kanzidata ya uzalishaji wa ng’ombe wa maziwa, matumizi ya ng’ombe bora wa maziwa ili kufikia tija zaidi kiuchumi na kuanzishwa kwa jukwaa la kidigitali la ukusanyaji wa taarifa za uzalishaji na kutoa mrejesho.
Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa mradi wa ADGG Tanzania Dkt. Daniel Komwihangilo amesema mradi huo unaodhaminiwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates unatekelezwa pia katika nchini mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania lengo likiwa ni kuhakikisha tasnia ya maziwa inakua.
Dkt. Komwihangilo amebainisha kuwa kwa sasa mradi unaingia awamu ya tatu ambapo serikali iko katika kampeni ya Sensa ya Watu na Makazi, ambapo utunzaji wa takwimu au kutuzitunza katika njia zisizo sahihi husababisha sekta ya mifugo kushindwa kukua zaidi.
Mradi wa Kuboresha Mbari za Ng’ombe wa Maziwa nchini (ADGG) unaotekelezwa na Taasisi ya Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) unaingia awamu ya tatu na na tayari unatekelezwa katika halmashauri nane katika mikoa mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba akifungua warsha ya wadau wa ng’ombe wa maziwa kupitia Mradi wa Kuboresha Mbari za Ng’ombe wa Maziwa nchini (ADGG) unaotekelezwa na TALIRI kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Mbeya, ambapo mradi huo umeingia awamu ya tatu hapa nchini. Prof. Komba amesema serikali ipo katika hatua muhimu za utekelezaji wa mradi kwa kuboresha maeneo kadhaa ili mradi huo kuwa na tija zaidi kwa wafugaji. Mradi wa ADGG unadhaminiwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates katika nchi mbalimbali barani Afrika. (05.08.2022)
Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Kuboresha Mbari za Ng’ombe wa Maziwa nchini (ADGG) Dkt. Daniel Komwihangilo unaodhaminiwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates akizungumza wakati wa warsha ya wadau wa ng’ombe wa maziwa kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Mbeya, ambapo amesema ni muhimu kutunza takwimu za mifugo ili kukuza sekta hiyo. Mradi wa ADGG unatekelezwa hapa nchini na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) katika halmashauri nane kwenye mikoa mbalimbali nchini. (05.08.2022)
Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mbari za Ng’ombe wa Maziwa nchini (ADGG) Dkt. Eliamoni Lyatuu unaodhaminiwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates akizungumza wakati wa warsha ya wadau wa ng’ombe wa maziwa katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Mbeya. Mradi wa ADGG unatekelezwa hapa nchini na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) katika halmashauri nane kwenye mikoa mbalimbali nchini. (05.08.2022)
Mtafiti Mkuu wa Mradi wa Kuboresha Mbari za Ng’ombe wa Maziwa nchini (ADGG) Bw. Gabriel Msuta unaodhaminiwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates akifafanua hoja mbalimbali wakati wa warsha ya wadau wa ng’ombe wa maziwa katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Mbeya. Mradi wa ADGG unatekelezwa hapa nchini na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) katika halmashauri nane kwenye mikoa mbalimbali nchini. (05.08.2022)
Baadhi ya washiriki wakisikiliza hoja mbalimbali kutoka kwa wahamasishaji wakati wa warsha ya wadau wa ng’ombe wa maziwa kupitia Mradi wa Kuboresha Mbari za Ng’ombe wa Maziwa nchini (ADGG) katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Mbeya. Mradi huo unadhaminiwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates na unatekelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) katika halmashauri nane kwenye mikoa mbalimbali nchini. (05.08.2022)
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba na baadhi ya washiriki kwenye warsha ya wadau wa ng’ombe wa maziwa kupitia Mradi wa Kuboresha Mbari za Ng’ombe wa Maziwa nchini (ADGG) iliyofanyika katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Mbeya. Mradi huo unadhaminiwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates na unatekelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) katika halmashauri nane kwenye mikoa mbalimbali nchini. (05.08.2022)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni