Nav bar

Jumapili, 14 Agosti 2022

MATUKIO KATIKA PICHA KWENYE MAONESHO YA NANENANE AGOSTI 6, 2022

 


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Tixon Nzunda (wa pili kutoka kushoto) akikagua malisho ya mifugo yanayopatikana katika viwanja vya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya, mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kutoa wito wa kuwepo elimu zaidi kwa wafugaji juu ya ulimaji wa malisho. (06.08.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Tixon Nzunda (kushoto) akikagua mifugo ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) inayopatikana katika viwanja vya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya, mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuitaka NARCO kuhakikisha inaboresha zaidi mifugo yake na kutoa elimu kwa wafugaji kuwa na mifugo michache na yenye tija. (06.08.2022)



Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Tixon Nzunda (kulia) akikagua nguruwe na kupewa taarifa namna nguruwe jike anavyopandikizwa mimba kwa njia ya uhimilishaji alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja kwenye viwanja vya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya na kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya mifugo. (06.08.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Tixon Nzunda (kushoto) akizungumza na mmoja wa wadau wa sekta ya mifugo juu ya ubora wa ngozi za mifugo katika kutengenezea bidhaa mbalimbali vikiwemo viatu mara baada ya Katibu Mkuu Nzunda kufanya ziara ya kikazi ya siku moja kwenye viwanja vya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya na kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya mifugo. (06.08.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah (wa nne kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Nazael Madalla (kushoto kwake) namna wanavyowafundisha wananchi njia mbalimbali za ufugaji samaki, wakati Dkt. Tamatamah alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja kukagua banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye viwanja vya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya. Kushoto kwa Dkt. Madalla ni Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Bw. Emmanuel Bulayi. (06.08.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akikagua ubora wa bwawa la kisasa la kufugia samaki wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja kukagua banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye viwanja vya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya. (06.08.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah akiwa ameshika moja ya vifaa vinavyotumika kuhifadhia samaki hai wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja kwenye viwanja vya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya na kutembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo ametaka wananchi wapatiwe elimu zaidi juu ya ufugaji samaki (06.08.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza na baadhi ya wadau wanaouza mazao ya uvuvi wakiwemo dagaa wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja kwenye viwanja vya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya na kutembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuwataka kuzidi kujiimarisha kibiashara ili kunufaika zaidi na biashara ya mazao ya uvuvi. (06.08.2022)



Kaimu Katibu Mkuu wa sekta ya Mifugo, Dkt. Charles Mhina akisaini kitabu cha Wageni (06.08.2022) muda mfupi baada ya kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya wakulima nanenane, kanda ya Mashariki yanayoendelea kufanyika Mkoani Morogoro.


Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mifugo, Dkt. Charles Mhina akiangalia kiatu kilichotengenezwa kwa Ngozi kwa mdau wa Ngozi Bi Kansilda Makwaila kutoka kampuni ya Kungwana Shoes Product, alipoenda kutembelea banda la Wizara ya Mifugo kwenye maonesho ya wakulima nanenane, yanayoendelea kufanyika mkoani Morogoro, Agosti 06,2022, (kulia) ni Afisa Uvuvi kutoka Idara ya Utafiti, mafunzo na huduma za Ugani-(DRTE uvuvi) Bi. Kresensia Mtweve.


Afisa Mifugo kutoka Shamba la Kuzalisha Mifugo Ngerengere, Bi Mwansiti Zuberi (wa kwanza kulia) akionyesha na kuelezea aina za Ngo'mbe wanaopatikana kwenye shamba hilo, kwa Kaimu Katibu Mkuu wa sekta ya Mifugo, Dkt. Charles Mhina, alipofika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwenye maonesho nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea kufanyika mkoani Morogoro Agosti 06,2022.


Kaimu Katibu Mkuu wa sekta ya Mifugo, Dkt. Charles Mhina, akiwa ameshika zao la mwani wakati alipokuwa akipatiwa maelekezo na faida ya mwani kutoka kwa Afisa Uvuvi, Bi Fatma Juma, alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea kufanyika Mkoani Morogoro, Agosti 06,2022.


Afisa Mazingira kutoka kitengo cha Mazingira, Bi Joyce Kasebele,(wa kwanza kulia), akimuelezea Kaimu Katibu Mkuu wa sekta ya Mifugo, Dkt. Charles Mhina, kuhusu kazi zinazotekelezwa na kitengo cha mazingira ili kuhakikisha malisho ya Mifugo yanapatikana kwa wingi, alipotembelea banda la maonesho ya wakulima nanenane, Mkoani Morogoro, Agosti 06,2022.

Nahodha kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Nyegezi Mwanza, Bw.  Edward Maeja (kulia) akitoa elimu ya nyavu zisizo sahihi  na nyavu sahihi za uvuvi kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kujifunza mambo mbalimbali wakati wa maonesho ya nanenane yanayofanyika kwenye kiwanja cha Nyamhongolo Mkoani  Mwanza, Agosti 06, 2022.


Daktari wa Mifugo kutoka bodi ya nyama Tanzania (TMB) Kanda ya ziwa, Dkt. Msomi Antony akiongea na wadau wa nyama (hawapo pichani) walipotembelea banda Hilo kwenye uwanja wa Nyamhongolo wakati maonesho ya nanenane Mkoani Mwanza, Agosti 06, 2022

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni