Nav bar

Jumapili, 14 Agosti 2022

MATUKIO KATIKA PICHA KWENYE MAONESHO YA NANENANE AGOSTI 7, 2022

 

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein A. Kattanga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kwenye Banda la Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzani (TVLA) lililopo ndani ya banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi alipotembelea kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wakala siku ya tarehe 07/08/2022 kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale. Waliosimama nyuma yake kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Rashid Tamatamah na aliesimama mbele yake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dkt. Stella Bitanyi.


Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein A. Kattanga akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda kuhusiana na Wizara ilivyojipanga kupunguza vifo vya Mifugo kwa kutumia chanjo zinazozalishwa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa kufuata ratiba ya kitaifa ya uchanjaji wa Mifugo inayoratibiwa na Wizara siku ya tarehe 07/08/2022 alipotembelea banda la Wakala lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale.


Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga (wapili kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo wa Shirika lisilo la kiserikali la Heifer International, Ndugu Mark Tsoxo juu ya kazi zinazofanywa na Shirika hilo alipotembelea Banda la Wadau hao wa Tasnia ya Maziwa Nchini leo Agosti 7, 2022 kwenye maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya, aliyesimama mwisho upande wa kushoto ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akizungumza na wadau wa mifugo na uvuvi mubashara kupitia Mashujaa FM mkoani Lindi wakati wa Maeonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kwenye Viwanja vya Ngongo. (07.08.2022)

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe (kushoto) akisikiliza jambo kwa makini kutoka kwa Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya walipokutana mara baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein A. Kattanga kuwasili kwenye Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo Agosti 7, 2022 kwenye maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya.

Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali za vyakula vya Mifugo, Bw. Rogers Shengoto kutoka Idara ya uendelezaji malisho na Rasilimali za vyakula vya mifugo (DGLF) akimuonyesha dawa za Mifugo zinazouzwa na Kampuni inayouza madawa ya mifugo ya Rol- Agrovet, Mgeni rasmi Katibu uenezi na Itikadi CCM Taifa Mhe. Shakha A. Shakha alipotenbelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya wakulima nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea kufanyika mkoani Morogoro.

Mkurugenzi msaidizi kutoka kitengo cha rasilimali za vyakula vya mifugo, (DGLF) Bw. Rogers Shengoto, akimuonyesha aina mbalimbali za mbegu na malisho ya mifugo yanayozalishwa kutoka shamba la Vikuge- Kibaha, Mgeni Rasmi wa maonesho ya nanenane kanda ya mashariki, Katibu uenezi na Itikadi CCM Taifa, Mhe. Shakha A. Shakha, alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya wakulima nanenane, yanayoendelea Mkoani Morogoro, Agosti 7,2022.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi chuo cha Uvuvi nyegenzi (wa pili kutoka kushoto kwake) namna wanavyowafundisha wananchi njia mbalimbali za ufugaji samaki,  alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya nanenane yanayofanyika kwenye kiwanja cha Nyamhongolo Mkoani Mwanza, Agosti 07, 2022.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima (kulia) akipata maelezo juu ya mabondo na faida zake kutoka kwa Mkufunzi chuo cha Uvuvi nyegenzi Bw. Edward Maeja alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Nyamhongolo Mkoani Mwanza Agosti 07, 2022.

Fundi mchundo kutoka Taasisi ya utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Bi. Zena Abdi akitoa elimu kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Nyamhongolo Mkoani Mwanza Agosti 07, 2022.

Msimamizi wa mabwawa kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Moabu Msukwa (kushoto) akitoa elimu ya ufugaji wa samaki kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Nyamhongolo Mkoani Mwanza Agosti 07, 2022.

Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya (katikati) akijadili jambo na Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania, Dkt. Daniel Mushi walipokutana leo Agosti 7, 2022 kwenye maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya, upande wa kulia ni Mteknolojia wa Chakula wa Bodi ya Maziwa kanda ya Nyanda za juu kusini, Ndugu Kennedy Daniel.

Afisa Utafiti wa Mifugo, kutoka Wakala wa Maabara Tanzania (TVLA) Bw. Henry Mlundachuma akitoa elimu  kwa wadau kuhusu Teknolojia ya upimaji  wa ubora wa vyakula vya mifugo kwenye maabara hiyo walipotembelea banda la  Wizara ya Mifugo, kwenye maonesho ya wakulima nanenane kanda ya Mashariki  yanayoendelea kufanyika Mkoani Morogoro, Agosti 07,2022.

Afisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Hamady  Makorwa (kulia) akitoa elimu kuhusu aina na athari za Uvuvi haramu kwa wadau wa uvuvi waliofika kwenye banda la Wizara hiyo lililopo kwenye Maonesho ya Nanenane kanda ya kati yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma leo (07.08.2022).

Mtaalam wa Uvuvi Bw.Hamis Athaman akiwa katika banda la Monesho ya Wakulima Nanenane katika kituo cha Kanda ya Magharibi Viwanja vya Ipuli kutoka Kambi ya Magereza ya Kwiranga mkoani Kigoma akionesha tekinolojia ya Ufugaji Mseto wa Samaki kwa wadau wa  kuwa na bwawa na banda la ufugaji kuku katika eneo hilo pembeni mwa bwawa ambapo kuku watakuwa wanafugwa itapatikana  samadi itakuwa inadondokea kwenye  maji na kurutubisha yale maji ambayo yatakuwa chakula cha samaki kilicho bora zaidi na yale maji ya bwawa yatakuwa ya rangi ya kijani cheusi.Ufugaji huo   unafaida kwa maeneo ambayo ni madogo ya kufanyashghuli mbalimbali aidha faida nyingine ya ufagaji ea namna hii wa kuku na samaki kuwa katika eneo moja unapata chakula cha samaki na unapata mayai na kuku wa nyama pia.(07.08.2022)


Mtaalam wa Mifugo toka Banda la magereza Bw.Kulwa Charles akiwa kwenye  maonesho ya Nanenane kituo cha kanda ya Magharibi mkoni Tabora, viwanja vya Ipuli kutoka Wilaya  ya Kibondo Mkoani Kigoma ammeleta tekinolojia  bora ya ufugaji wa ng'mbe Chotara ambayo inatija kwa wafugaji wa kanda ya Magharibi  kama watakubali ushauri watakaopewa na mtaalam kuhusu matumizi ya tekinolojia ya ufugaji wa ng'mbe hao wenye sifa ya kuvumilia magonjwa , gharama ndogo za kuwatunza,wenye uwezo mkubwa wa kuzalisha mazao mengi na bora ambayo yatampatia mfugaji na Taifa tija ya kipato (07.08.2021)


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akiongea na Wafugaji katika Wilaya Urambo Mkoani Tabora kwa lengo la kutatua kero za Wafugaji wa Wilaya hiyo zinzao wakabili ikiwa ni uhaba wa Malisho hususan wakati wa kiangazi, Ukosefu wa maji ya kunyweshea Mifugo,upungufu wa Maafisa ugani,ukosefu wa Malambo,visima na majosho ya kuogeshea mifugo dawa ya josho, Mheshimiwa Waziri Ndaki akitoa ufafanuzi kujibu kero zao amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza Bajeti ya Mifugo  ili kuboresha shughuli za Wakulima na Wafugaji ambapo kila mwaka bajeti hiyo ilikuwa kidogo na haitoshi kuhudumia shughuli za wakulima na wafugaji ili ziwe na tija,hivyo kuanzi kipindi cha kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu tutanza kampeni za kutoa elimu ya mikikutano  kwa wafugaji nchi nzima kuelekea kwenye ufugaji kibiashara,suala la malisho tutalivalia njuga kwa kwa kuwa ndiyo kiini cha ugomvi kati wakulima na wafugaji.Kila mfugaji lazima apatiwe eneo la malisho amilikishwe na aliendeleze na kulindwa.Aidha tutaboresha majosho 07.08.2022


Mtaalam wa Mifugo toka banda la maonesho la magereza ya Bangwe akiwa kanda ya Magharibi viwanja vya Ipuli Mkoani Tabora Bw.Charles Francis akionesha uzalishaji wa malisho bora ya Mifugo na kuandaa malisho hayo kama hei kwa ajili ya kutumia wakati wa kiangazi.Malisho hayo ni ya aina ya Guatemala,Guenea grass,Ellephant grass, na jamii ya mikunde ambayo ni pamoja na  Demodium, Lablab purpureus.Malisho hayo yanaandaliwa kiutalaam kwa kwa kushauriwa kila mfugaji amiliki eneo lisajiliwe na aboreshe eneo lake kwa kufuata taratibu za kilimo bora cha kustawisha malisho aidha awe na taratibu wa kulisha mifugo yake kwa mzunguko katika  " padocks zake " na mengine aweze kuhifadhi katika banda lake kwa mtindo wa hei.(07.08.2022).

Daadhi ya wafugaji kwa nyakati tofauti wakieleza kero zao wamesema wanaomba kujengewa Chuo cha Mifugo ili wafugaji na watotoa wao wapate elimu ya ufugaji wasaidie kuboresha hali ya ufugaji katika wilaya yao yenye Mifugo Mingi hapa nchini. (07.08.2022)





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni