Daktari wa Wakala ya Veterinari Wa Mifugo kituo cha Tabora Kanda ya Magharibi Dkt.Husna Kassuku (kushoto) akitoa maelezo ya umuhimu wa matumizi ya chanjo za Mifugo zinazonyeshwa katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika viwanja vya Ipuli kwenye Maonesho ya wakulima ,Wafugaji na wavuvi yanayoendelea katika viwanja hivyo ambapo amesema lengo la kuonyesha chanjo hizo ni kutoa fursa wafugaji kijifunza tekinolojia mbalimbali za mifugo ikiwemo chanjo zinazosaidia kuboresha shughuli za ufugaji nakuwa zenye tija,hivyo kupunguza gharama na hasara zitokanazo na kutibu Mifugo inapougua au kumpoteza mnyama kwa kifo.(04.08.2022).
Picha ya pamoja ya baadhi ya washiriki wa Monesho ya Nanenane, 2022 katika kituo cha Tabora Kanda ya Magharibi viwanja vya Ipuli nje kidogo ya mji wa Tabora. (04.08.2022)
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ukaguzi na Haki za Wanyama, Dkt. Annette Kitambi akiendelea na zoezi la utambuzi wa Mifugo alipotembelea banda la Halmashauri ya Babati lililopo kwenye maonesho ya Wakulima NaneNane Kanda ya Kaskazini yanayoendelea Mkoani Arusha Agosti 4, 2022.
Mkufunzi, Wakala ya Mafunzo ya Mifugo Kampasi ya Tengeru (LITA), Bi. Teresia Teti (kushoto) akimpatia vipeperushi mdau wa Mifugo alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Wakulima NaneNane Kanda ya Kaskazini yanayoendelea Mkoani Arusha Agosti 4, 2022.
Mkurugenzi Msaidizi Huduma Ukaguzi na Haki za Wanyama, Dkt. Annette Kitambi (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa wadau wa mifugo kuhusu huduma zinazotolewa katika Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya Wakulima NaneNane Kanda ya Kaskazini yanayoendelea kufanyika Mkoani Arusha Agosti 4, 2022. Wa kwanza kushoto ni Afisa wa Teknolojia, Habari na Mwasiliano(TEHAMA), Bw. Joseph Nkwabi.
Afisa Mifugo Mkuu, Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Bw. Israel Kilonzo (kushoto) akitoa elimu kwa wafugaji wa Kanda ya Kaskazini kuhusu umuhimu wa kulima malisho ya mifugo alipokutana na wafugaji hao waliotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye maonesho ya Wakulima NaneNane Kanda ya Kaskazini yanayoendelea Mkoani Arusha Agosti 4, 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni