Mratibu wa Sekta ya Uvuvi kitaifa kutoka Shirika la chakula na kilimo la umoja wa Mataifa (FAO), Bi. Olivia Mkumbo akieleza umuhimu wa jukwaa la wanawake ikiwa ni pamoja na kuwaleta wanawake pamoja, kuwawezesha kiuchumi kupitia Uvuvi Ili kuinua kipato cha familia na kuondokana na umaskini Agosti 03, 2022 Mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Kitaifa kinachoratibu Muongozo wa Kuendeleza Uvuvi Mdogo nchini (NTT), Bw. Yahya Mgawe (picha ya juu) na Afisa Mfawidhi usimamizi wa rasilimali za Uvuvi Kanda kuu ya ziwa Tanganyika, Bw. Juma Makongoro (picha ya chini) wakichangia hoja wakati wa mafunzo ya masuala ya kijinsia kwa wanawake wanaojihusisha na uchakataji wa mazao ya Uvuvi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa "the wallet " mkoani Kigoma, Agosti 03, 2022.
Mteknolojia wa samaki Mkuu, Bi. Flora Ruhanga akichangia hoja wakati wa mafunzo ya masuala ya kijinsia kwa wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania (TAWFA) Mkoani Kigoma Agosti 03, 2022.
Mtaalam wa masuala ya jinsia kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la umoja wa Mataifa (FAO) Nchini Ghana, Bi. Clara Park (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na waratibu wa mafunzo ya wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania (TAWFA) na sehemu ya wanawake hao nje ya ukumbi wa "the wallet" Mkoani Kigoma Agosti 03, 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni