Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), akizungumza na
Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber wakati balozi huyo alipofika
katika ofisi za wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma na kuelezea nia ya
makampuni mbalimbali kuwekeza nchini Tanzania katika Sekta ya Mifugo kwa
kuingia mikataba ikiwemo ya kuwekeza kwenye ranchi za taifa. Aliyekaa kulia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda. (16.08.2022)
Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki
(Mb), Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber na Katibu Mkuu wa
wizara hiyo anayeshughulikia Mifugo Bw. Tixon Nzunda (kulia), wakati balozi
huyo alipofika katika ofisi za wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma kuzungumzia
masuala mbalimbali ya uwekezaji wa makampuni ya Misri katika Sekta ya Mifugo
hapa nchini. (16.08.2022)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo (Uvuvi) Dkt.
Rashid Tamatamah (kushoto), akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Misri nchini
Tanzania Mhe. Mohamed Gaber, Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Bw. Emmanuel Bulayi
na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Nazael Madalla juu ya
uwekezaji katika Sekta ya Uvuvi, mara baada ya balozi huyo kufika katika ofisi
za wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma. (16.08.2022)
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah
Ulega (Mb), (wa tatu kutoka kulia), Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe.
Mohamed Gaber, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah
(wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Bw. Emmanuel Bulayi (wa
kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Nazael Madalla
(wa kwanza kushoto), mara baada ya mazungumzo juu ya uwekezaji katika Sekta ya
Uvuvi hapa nchini. (16.08.2022)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni