Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, Mej. Jen. Suleiman Mzee amewataka Wataalam wa Mifugo wa Jeshi hilo
kutumia Mafunzo ya Usajili na Uwekaji wa alama za Utambuzi wa Mifugo kwenda
kuongeza tija ya uzalishaji katika maeneo wanayotoka.
Kamishna Jenerali Mzee ameyasema
hayo leo (10.06.2022) wakati akifungua Mafunzo ya Usajili na Uwekaji wa alama
za Utambuzi wa Mifugo kwa Wataalam wa Mifugo wa Jeshi la Magereza yaliyofanyika
kwenye Ukumbi wa Meja Jenerali Suleiman Mzee - Msalato Jijini Dodoma.
“Usajili na Uwekaji wa Alama za
Utambuzi kwa mifugo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza kutasaidia Jeshi kuwa na
taarifa sahihi za idadi ya mifugo ikiwa ni pamoja na kulinda mifugo hiyo,”
alisema
Jeshi la Magereza limekuwa
likipata changamoto ya taarifa sahihi za uzalishaji wa mifugo na mazao yake,
hivyo kwa kutumia njia hii ya usajili na utambuzi kutasaidia sana hata kwenye
usimamizi wa uzalishaji wa mifugo pamoja na mazao yake.
Aidha, amewapongeza waataalam hao
wa mifugo kwa kazi nzuri ambayo wanayoifanya kwani kwa sasa mifugo katika Jeshi
hilo imeanza kuongezeka. Vilevile amewasihi wataalam hao kuhakikisha wanaongeza
jitihada zaidi katika usimamizi wa uzalishaji wa mifugo na mazao yake. Pia
amewataka wataalam hao pamoja na viongozi wao kwenye maeneo wanayotoka kuongeza
ubunifu katika uzalishaji.
Naye Afisa Utambuzi kutoka Wizara
ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Mifugo), Dkt. Gibonce Kayuni amesema kuwa usajili na
utambuzi wa mifugo kwa njia ya kielektroniki una faida nyingi ikiwemo ya kuwa
na taarifa sahihi za takwimu za mifugo kitu kitakachosaidia katika upangaji wa
mipango ya maendeleo ya mifugo. Pia zoezi hili litasaidia kupunguza tatizo la
wizi wa mifugo na kuwawezesha wafugaji kupata bima itakayowawezesha kukopesheka
kwenye taasisi za fedha.
Mkurugenzi wa Sehemu ya Kilimo, Mifugo na Utunzaji wa Mazingira, ACP.
Rocky Mbena amesema kuwa kwa sasa Magereza inaendelea na uboreshaji wa Kosaafu
za Mifugo ili kuwa na mifugo itakayozalisha kwa tija. Lakini pia wanaendelea na
uboreshaji wa mahusiano na wadau mbalimbali wa mifugo kwa lengo la kuongeza
tija kwenye uzalishaji.
Afisa Utambuzi wa Mifugo kutoka WMUV, Dkt. Gibonce Kayuni (kushoto) akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Maj. Jen. Suleiman Mzee nakala ya Mwongozo wa Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo mara baada ya kufungua mafunzo ya Usajili na Uwekaji wa alama za Utambuzi wa Mifugo kwa Wataalam wa Mifugo wa Jeshi la Magereza yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Meja Jenerali Suleiman Mzee Msalato Jijini Dodoma. (10.06.2022)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Maj. Jen. Suleiman Mzee akifungua mafunzo ya Usajili na Uwekaji wa Alama za Utambuzi kwa Mifugo kwa Wataalam wa Mifugo wa Jeshi la Magereza yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Meja Jenerali Suleiman Mzee Msalato Jijini Dodoma. (10.06.2022)
Afisa Utambuzi wa Mifugo kutoka WMUV, Dkt. Gibonce Kayuni akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya Usajili na Uwekaji wa alama za Utambuzi wa Mifugo kwa Wataalam wa Mifugo wa Jeshi la Magereza yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Meja Jenerali Suleiman Mzee Msalato Jijini Dodoma. (10.06.2022)
Afisa TEHAMA kutoka WMUV, Bw. Joseph Mkwabi akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya Usajili na Uwekaji wa alama za Utambuzi wa Mifugo kwa Wataalam wa Mifugo wa Jeshi la Magereza yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Meja Jenerali Suleiman Mzee Msalato Jijini Dodoma. (10.06.2022)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Maj. Gen. Suleiman Mzee akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Mifugo) na Wataalam wa Mifugo wa Jeshi la Magereza mara baada ya kufungua mafunzo ya Usajili na Uwekaji wa alama za Utambuzi wa Mifugo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Meja Jenerali Suleiman Mzee Msalato wilayani Chamwino mkoani Dodoma. (10.06.2022)
Kamishna Generali wa Jeshi la Magereza, Maj. Gen. Suleiman Mzee akimvisha hereni moja wa ng’ombe wa Jeshi la Magereza mara baada ya kufungua Mafunzo ya Usajili na Uwekaji wa alama za Utambuzi wa Mifugo kwa Wataalam wa Mifugo wa Jeshi la Magereza yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Meja Jenerali Suleiman Mzee Msalato Jijini Dodoma. (10.06.2022)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni