SERIKALI kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, sekta ya Mifugo inatarajia kuanza kutumia mfumo mpya wa utoaji vibali kwa njia ya kielekroniki kusafirisha mifugo na bidhaa zote zitokanazo lengo likiwa ni kuondoa urasimu, vitendo vya rushwa na uzembe uliokuwa unafanywa na baadhi ya wataalam wanaoshughulikia upatikanaji wa vibali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Bw. Tixon Nzunda, amesema kuwa mfumo huo wa kielekroniki utaanza kutumika rasmi Julai mosi mwaka huu. aliyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya mfumo mpya wa kielektroniki unajulikana kama "Mifugo Integrated Management Information System" (MIMIS).16 Juni 2022. Jijini Mbeya.
Nzunda,Alisema mfumo huo utarahisisha shughuli za utoaji vibaji kwa njia ya mtandao ambapo wafanyabiashara hawatapanga tena foleni kwa wataalam wakiwamo maofisa ugani kushughulikia vibali vya kusafirisha mifugo na mazao yatokanayo na mifugo badala yake watatumia teknolojia za simu na kompyuta kupata vibali.
Amesema Serikali ilianzisha mfumo huo ukiwa na lengo la kuokoa na kukusanya mapato yatokanayo na ukataji wa vibali sambamba na kuwabana watumishi waliokuwa wakiendekeza rushwa na urasimu kuwahudumia wananchi.
“Tunajivunia kuona sasa tumefanikiwa kuanzisha mfumo wa kielekroniki ambao utatumika kutoa vibali vya usafirishaji wa mifugo na bidhaa zake, kama vile ngozi, mayai na nyama kutoka kila pembe ya nchi huko aliko nakupata kibali chake kupitia simu yake ya mkononi na kuendelea na shughuli zake,” alisema Nzunda.
Aliongea kuwa serikali imeamua kuutambulisha mfumo huo kwa Mikoa ya Nyanda za juu kusini hususani mkoani Mbeya kwa kuwa ni eneo ambalo linawafugaji wengi ambao wanafuga kisasa na kuzalisha maziwa yenye ubora unaokubalika kimataifa.
Kwa upande wake, Msajili wa Bodi ya Nyama nchini, Dkt. Daniel Mushi, alisema mfumo huo utawarahisishia wafanyabiashara wa nyama nchini kupata vibali kwa wakati na kuweza kufanya shughuli zao kwa uhuru.
Alisema mfumo huo utapunguza mlolongo mrefu wa kufuatilia vibali katika ofisi za serikali na badala yake vitakatwa kielekroniki.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Trade Mark East Afrik, Lilian Masalu alisema walishawishika kuisaidia serikali kuanzisha mfumo huo baada ya kuona ucheleweshwaji wa vibali vya kusafirisha mifugo hali iliyokuwa inasababisha bidhaa zitokanazo na mifugo kuharibika na wafanyabiashara kuingia hasara.
Alisema mfumo huo utakuwa na tija kwa mfugaji na mfanyabiashara ambao kwa pamoja wataweza kuuza kwa wakati na kujiingizia kipato.
Baadhi ya wafanyabiashara wanaojishughulisha na uuzaji wa ngozi walisema mfumo wa huo wa kuomba vibali kielekroniki utasaidia kuwa na bei ya pamoja nchini kuliko ilivyo sasa ambapo kila Wilaya ilikuwa unapanga bei zake za kuomba vibali.
Msajili wa bodi ya nyama nchini, Dkt. Daniel Mushi, akizungumza na wadau wa sekta ya mifugo wa kanda ya mkoa wa Mbeya, wakati alipokuwa akihitimisha mafunzo ya mfumo mpya wa kielektroniki wa usimamizi wa utoaji vibali mbalimbali vya kusafirishia mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchini, ambapo amewashukuru wadau hao kwa kushiriki vyema katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Royal Tughimbe Hotel, Jijini Mbeya, 16 Juni 2022.
Sehemu ya wadau wa sekta ya mifugo wa mkoa wa mbeya ambao ndio wasindikaji wa maziwa, wachunaji wa Ngozi, wafugaji na wasafirishaji wa mazao ya mifugo, walioshiriki kwenye mafunzo ya mfumo mpya wa kielektroniki (MIMIS) wakisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa mwezeshaji wa mafunzo ya mfumo huo, (hayupo pichani) wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Royal Tughimbe Hotel, Jijini Mbeya,16 Juni 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni