Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2021

FISH4ACP ITACHOCHEA ONGEZEKO LA PATO LA TAIFA KUPITIA SEKTA YA UVUVI-DKT. TAMATAMAH

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah amesema kuwa Mradi wa FISH4ACP utasaidia kuongeza nguvu kwenye maboresho ambayo sekta ya Uvuvi inaendelea kuyafanya hivi sasa  kwa ajili ya  kuongeza mchango wa sekta  Dkt. Tamatamah ameyasema hayo   (06.12.2021) wakati akifungua warsha ya siku mbili ya ukamilishaji mpango wa maboresho ya mnyororo wa thamani wa dagaa na samaki aina ya mgebuka kutoka Ziwa Tanganyika iliyofanyika kwenye ukumbi wa “Kigoma Social Hall” uliopo Manispaa ya Kigoma. “Lakini pia mradi huu utakuwa na mchango mkubwa katika kutoa ajira hasa kupitia maboresho ya mnyororo wa thamani ya mazao yanayotoka  Tanganyika, utapunguza umasikini miongoni mwa wavuvi na wadau wote watakaohusika kwenye mnyororo huo na kubwa zaidi utaongeza kiwango cha ulaji wa samaki ambao kwa mujibu wa Shirika la Kilimo na Chakula Uliwenguni (FAO) kila Mtanzania anakula kiasi cha kilo 8.5 kwa mwaka hivyo naamini mpaka kukamilika kwa mradi huu angalau k...

WAFUGAJI WATAKIWA KUTUMIA MFUMO WA UTAMBUZI WA MIFUGO KIELEKTRONIKI

Picha
  Serikali imewataka wafugaji Wilayani Mufindi kutumia vyema fursa iliyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi   ya utambuzi wa mifugo kwa mfumo wa kielektroniki ili kuondokana na changamoto ya wizi wa mifugo hiyo uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara. Rai hiyo ilitolewa Disemba 4, 2021 na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Bw. Saad Mtambule wakati wa uzinduzi wa zoezi la utambuzi, usajili na ufatiliaji mifugo kwa kuweka hereni maalum sikioni zenye namba zinazotolewa na Wizara. Alisema katika kipindi cha hivi karibuni Wilaya hiyo ilikumbwa na wimbi la wizi wa Ng'ombe ambapo ilikuwa ni vigumu kutambua kutokana na kukosa Alama  maalum za kuwatambulisha. "Tulikuwa na changamoto ya wizi wa mifugo kwa muda mrefu sana na ilikuwa ni jambo gumu kutambua mifugo ikipotea katika kijiji kimoja na kuipata katika kijiji kingine kwa hiyo kupitia utambuzi huu utakuwa umekomesha kabisa wizi kwa sababu mifugo yote itakua inatambulika" alisema Akizungumzia mfumo huo wa utambuzi Mkurugen...