Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kitema wilayani Muleba Mkoa wa Kagera ambapo amewaeleza kuwa Mhe. Rais Samia Hassan ameridhia wabaki katika eneo hilo ambalo linamilikiwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) hivyo upimaji utafanyika upya na kuweka mipaka. (12.07.2021)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wataalam kutoka wizarani upande wa sekta ya Mifugo, sekretarieti ya mkoa wa Kagera, Wilaya ya Muleba, Chama cha Mapinduzi na wananchi wa Kijiji cha Katema mara baada ya kumalizika kwa mkutano ambapo wananchi wamekubaliwa kubaki kwenye makazi yao katika eneo linalomilikiwa na NARCO. (12.07.2021)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akisikiliza hoja zilizokuwa zikitolewa na Mbunge wa Muleba Kaskazini, Mhe. Charles Mwijage (aliyesimama) kwenye kikao kilichojadili mgogoro uliopo kati ya wananchi na NARCO kwenye Ranchi ya Mwesa II. Kulia ni Mbunge wa Muleba Kusini, Mhe. Dkt. Oscar Kikoyo. (12.07.2021)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni