Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewataka watendaji wa wizara hiyo ambao wanahusika na utungaji wa miongozo ya utafiti wa mifugo kuangalia namna ya kuweka adhabu kwa watafiti watakaoenda kinyume kwa kutofikisha tafiti zao kwa wafugaji ambao ndio walengwa wa utafiti.
Agizo hilo lilitolewa Aprili 14,
2020 na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Bedan
Masuruli wakati akizungumza na wadau wa sekta hiyo waliokutana jijini Dodoma
kwa ajili ya kujadili miongozo ya tafiti za mifugo iliyotolewa na Taasisi ya
Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI).
Alisema Wizara inatambua ugumu uliopo
katika kuweka adhabu kwa watafiti watakaoshindwa kufikisha tafiti zao kwa ajili
ya wafugaji lakini kitendo cha kutunga miongozo hiyo bila ya kuwa na sheria za
kuwabana kutasababisha kuchelewa kufikia malengo waliyojiwekea.
"Nataka nisisitize kwamba miongozo
hii tunayoijadili hapa mkaangalie namna ya kuweka na adhabu, japo naambiwa na
wanasheria kwamba haiwezekani lakini hatuwezi kuacha hivi kwa sababu tutachukua
hatua gani kama mtu hakufikisha matokeo ya utafiti kwa wafugaji au hata mtu
akiamua kutoa majibu ya uongo, ni muhimu iwepo ili tufikie lengo letu la mwaka
2025" alisema Dkt Masuruli
Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima alisema tayari sheria na
kanuni za kuhakikisha tafiti zinazofanyika zinatoka kabatini na kuwafikia
wafugaji na kwamba kinachofanyika sasa ni taasisi hiyo kufuatilia kila hatua ili
watafiti wazifikishe tafiti hizo kwa walengwa waliokusudiwa.
Alisema pamoja na mambo mengine taasisi
hiyo itahakikisha inashughulikia changamoto zote ikiwemo kuondoa vikwanzo
mbalimbali na kuweka mifumo rafiki ili kusaidia kuharakisha tafiti
zinazofanyika.
Naye mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Paulo Ochanga aliwataka wadau na watafiti
kuendelea kutilia mkazo tafiti zinazofanyika ili kukuza sekta ya mifugo nchini
ambayo inachangia pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 7 kwa sababu ya mazao ya
mifugo kuwa na thamani kubwa katika mnyororo wa thamani.
Kaimu Katibu Mkuu anayesimamia Sekta ya Mifugo, Dkt. Bedan Masuruli (aliyekaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Mifugo mara baada ya kikao cha kujadili miongozo ya utekelezaji wa kanuni za utafiti wa Mifugo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. (14.04.2021)Kaimu Katibu Mkuu anayesimamia Sekta ya Mifugo, Dkt. Bedan Masuruli akiongea na wadau wa Mifugo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kujadili miongozo ya utekelezaji wa kanuni za utafiti wa Mifugo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. (14.04.2021)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima akifafanua jambo wakati wa kikao cha kujadili miongozo ya utekelezaji wa kanuni za utafiti wa Mifugo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. (14.04.2021)
Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Paulo Ochanga akichangia hoja kwenye kikao cha wadau cha kujadili miongozo ya utekelezaji wa kanuni za utafiti wa Mifugo kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. (14.04.2021)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni