Nav bar

Jumatatu, 19 Aprili 2021

DKT. TAMATAMAH AFUNGUA WARSHA YA WADAU WA TASNIA YA UKUZAJI VIUMBE MAJI

 

Katibu Mkuu,Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akiongea na wadau wa Ukuzaji Viumbe Maji wakati akifungua Warsha ya Wadau wa Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji ya Kupokea na Kujadili Matokeo ya Utafiti wa Kutathmini Uzalishaji wa Samaki kwenye Mabwawa na Vizimba pamoja na Washiriki kwenye Mnyororo Mzima wa Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji iliyoandaliwa na Chama Kikuu cha Wakuzaji Viumbe Maji Tanzania (AAT) ambapo alisisitiza kuwa ushiriki wa Sekta binafsi katika ukuzaji viumbe maji utasaidia nchi kuondokana na changamoto ya upatikanaji samaki na kuondoa uvuvi haramu. Warsha hiyo inafanyika Mkoani Mwanza  leo Aprili 16, 2021.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) akiongea na Mdau wa Ufugaji Samaki Mkoani Mwanza, Meck Sadiki muda mfupi baada ya kufungua Warsha ya Wadau wa Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji ya Kupokea na Kujadili Matokeo ya Utafiti wa Kutathmini Uzalishaji wa Samaki kwenye Mabwawa na Vizimba pamoja na Washiriki kwenye Mnyororo mzima wa Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji inayofanyika Mkoani Mwanza leo Aprili 16, 2021.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa tatu kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Warsha ya Wadau wa Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji ya Kupokea na Kujadili Matokeo ya Utafiti wa Kutathmini Uzalishaji wa Samaki kwenye Mabwawa na Vizimba pamoja na Washiriki Kwenye Mnyororo Mzima wa Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji inayofanyika Mkoani Mwanza leo Aprili 16, 2021.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Wakuzaji Viumbe Maji Tanzania (AAT), Charles Maika akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha, Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa tatu kutoka kulia) kufungua Warsha ya Wadau wa Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji ya kupokea na kujadili matokeo ya utafiti wa kutathmini Uzalishaji wa Samaki kwenye Mabwawa na Vizimba pamoja na Washiriki kwenye Mnyororo mzima wa tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji inayofanyika Mkoani Mwanza leo Aprili 16, 2021.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni