Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akipewa maelezo na Mfanyakazi wa Kampuni ya Abajuko,
Mbarouk Masoud kuhusu Samaki aina ya Kambakochi katika banda la Kampuni ya
Abajuko alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya
Kimataifa ya 44 ya Sabasaba yanayofanyika katika Uwanja wa Mwl. Nyerere,
Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Julai 3, 2020.
Mkurugenzi wa Tanzania
Livestock Research Institute (TALIRI) Kanda ya Mashariki, Dkt. Zabron
Nziku(kushoto) akitoa maelezo kuhusu Mbegu na Malisho ya Mifugo kwa Mdau wa
Mifugo aliyetembelea banda la TALIRI leo Juni 3, 2020 katika Maonesho ya
Kimataifa ya 44 ya biashara ya Sabasaba yanayofanyika katika Uwanja wa Mwl.
Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Huduma za Ugani (WMUV), Dkt. Angelo Mwilawa (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mtaalam wa Ufugaji wa Samaki wa Kampuni ya Bigfish, Florence Mahimbo(kushoto) katika banda la Kampuni hiyo alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Kimataifa ya 44 ya Sabasaba yanayofanyika katika Uwanja wa Mwl. Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Mapema leo Juni 3, 2020.
Wadau wa Mifugo na Uvuvi
wakionesha kuvutiwa na Aquarium zilizopo katika banda la Wakala ya Elimu na
Mafunzo ya Uvuvi (FETA) walipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi
katika Maonesho ya Kimataifa ya 44 ya Sabasaba katika Uwanja wa Mwl. Nyerere,
Barabara Kilwa jijini Dar es Salaam Julai 3, 2020.
Mkurugenzi wa Idara ya
Utafiti na Huduma za Ugani(WMUV), Dkt. Angelo Mwilawa akisaini kitabu cha
wageni alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya
Kimataifa ya 44 ya Sabasaba yanayofanyika kwenye Uwanja wa Mwl. Nyerere,
Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Julai 3, 2020. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Utafiti na Huduma za Ugani (Uvuvi), Bw. Anthony Dadu. Kulia ni Watumishi wa
Wizara hiyo, wa kwanza ni Nyanzala Lupeja na wa pili ni Sebastian Shilangalila.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni