Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2017

SERIKALI YATAIFISHA KUNDI LINGINE LA NG'OMBE KUTOKA RWANDA

Picha
SERIKALI YATAIFISHA KUNDI LINGINE LA NG’OMBE KUTOKA RWANDA NA; MWANDISHI MAALUM – KASULU Kufuatia zoezi linaloendelea la oparesheni kamata mifugo linaloongozwa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, serikali kwa mara nyingine imetaifisha kiasi cha ng’ombe 171 waliokamatwa katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Akiongea katika zoezi hilo Waziri Mpina amesema Wilaya za mipakani mwa Nchi jirani ziko katika tishio kubwa la kuvamiwa na mifugo na kuelekeza mwanasheria wa Wilaya ya Kasulu kuanza kuandaa utaratibu wa mahakama kuzipiga mnada. “Hatua ya kwanza sisi kama Serikali tunataifisha ng’ombe hawa na kufanya utaratibu wa kuzipiga mnada na mwanasheria wetu wa Serikali aanze taratibu ambapo ng’ombe hao tutawapiga mnada kwa mujibu wa sheria ya magonjwa ya wanyama No. 17 ya mwaka 2003.” alisema Mpina. Mpina aliongeza kusema kuwa, ng’ombe hao kwa sasa wataendelea kuwa chini ya Serikali mpaka taratibu zitakapo kamilika, na kuitaka...

MHE WAZIRI LUHAGA MPINA AMETEKETEZA NYAVU ZINAZOTUMIKA KATIKA UVUVI HARAMU ZILIZOKAMATWA MKOANI KIGOMA

Picha
WAZIRI MPINA ACHOMA NYAVU KUKOMESHA UVUVI HARAMU NA MWANDISHI MAALUM KIGOMA Waziri wa Mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa Mkoani Kigoma zenye thamani ya shilingi Milioni thelalini na moja kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi hilo katika serikali hii ya awamu ya tano. Akiongea mara baada ya kuteketeza nyavu hizo hizo mapema leo, Mpina alionyesha kushangazwa na suala la uvuvi haramu kuwa sugu “kwa nini vita hii haina mwisho? Lazima yawezekana mbinu zinazotumika ni dhaifu ama silaha zinazotumika ni duni, ifike mahala suala hili   liwe historia”. Alisema Mpina. Akitoa Maelekezo kwa viongozi wa Mikoa ambayo shughuli hizi zinafanyika, Mpina aliwataka viongozi hao wawe na jukumu la kulinda rasilimali za taifa ikiwa ni mapoja na Bahari, Maziwa na mito. “kama nitashindwa kushughulia suala zima la uvuvi haramu, niitaaachia dhamana hii niliyopewa na Mheshimiwa Rais, na mpaka kufikia hatua hiyo lazima wengi watakuwa wamej...

MHE. WAZIRI ALIKUTANA NA WATUMISHI WA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMAIZI WA MAZINGIRA NEMC

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akitia saini katika kitabu cha wageni kwenye Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC   alipoenda kuagana nao na kutoa neno baada ya kufanya nao kazi kama Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara Mpya ya Mifugo na Uvuvi. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpinaakiwa katika mazungumzo na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza wakati wa kuagana na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, kulia ni mkaguzi wa Mazingirakanda ya Mashariki Bw. Jafari Chimgege na kushoto ni Dkt. Ruth Rugisha Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Baraza Picha ya Pamoja Waziri Mpina na baadhi ya watumishi wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC.

WAZIRI MPINA NA WAZIRI WA OMAN WAZUNGUMZIA MASUALA YA UWEKEZAJI WA VIWANDA KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

Picha
                                          NA MWANDISHI MAALUM W aziri anayeshughlia masuala ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amekutana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail na kujadili suala zima la uwekezaji wa viwanda katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi. Katika Mazungumzo hayo Waziri Mpina amemueleza   Waziri huyo wa uwekezaji wa Oman kuwa Tanzania imekuwa ikizalisha nyama kwa kiasi cha tani 36 kwa siku na imekuwa ikifanya biashara kwa kuuza tani za nyama ambazo hazijakatwa katika nchi za falme za kiarabu ikiwemo Oman.  Wakati umefika sasa kwa nchi hizi mbili kushirikiana kwa pamoja katika Sekta hii kwa Oman kuwekeza katika Viwanda vya ndani vya nyama kwa kuendeleza viwanda vilivyopo na hata kujenga Viwanda vipya, akitolea mfano ujenzi wa kiwanda cha...