MKUTANO WA MHE CHARLES TIZEBA WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI NA WAANDISHI WA HABARI 13/7/2016
Na ,GCU (Mifugo na Uvuvi)
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi leo hii amewasimamisha kazi maafisa waandamizi wakuu wa taasisi mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi baada ya kugundua kuwa kulikuwa na ukiukaji mkubwa katika taratibu za uendeshaji wa taasisi zao. Mhe. Waziri ametangaza haya wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Kilmo 1 jijini Dare es salaam leo hii 13/7/2016 .
|
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizemba akiongea na waandishi wa habari kulia kwake ni Katibu Mkuu (U) Dkt. Yohana Budeba
|
Alisema kwamba hali ya chakula kwa ujumla hapa nchini ni nzuri kwa ujumla pamoja na kuwa tathmini ya kiasi cha mazao yanayotakiwa kuvunwa bado haijafanyika. Alieleza kuwa kumekuwa na ununuzi mkubwa wa chakula kutoka kwa wakulima kabla ya kufanya tathmini ambapo ni kinyume na utaratibu. Ameagiza tathmini hii iwe imekamilika ndani ya wiki mbili.
Mhe. Waziri aliendelea kueleza kuwa amebaini kuwa kuna vibali vya kusafirisha mazao nje ya nchi ambavyo vimekuwa vikitolewa na mamlaka ya hifadhi ya chakula kinyume na utaratibu. Aliagiza vibali hivyo visitolewe tena hadi tathmini itakapofanyika, Aidha kutokana na ukiukaji wa taratibu hizo aliagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya usalama wa chakula nchini Bwana Ombeni Lemweli ili apishe uchunguzi na Mkurugenzi wa sera na Mipango wa sekta ya Kilimo ameteuliwa kukaimu nafasi hiyo.
Mhe. Waziri aliendelea kueleza kwamba amebaina kuwa kulikuwa na utunzaji mbovu wa nafaka katika maghala yake na hata mahindi yaliyoharibika hayakutolewa kibali cha kuyauza kama chakula cha mifugo kwa visingizio vya kutopata kibali cha TFDA NA TBS cha kuyauza, lakini baadaye ilibainika kwamba mahindi hayo hayakuwa mabovu aidha imebainika kwamba na kulilkuwa na ununuzi wa mahindi kiholela bila kuzingatia uwezo wa maghala yaliyopo, hali hii imesababisha hasara kubwa sana kwa Taifa.
Aidha imebainika kwamba walishindwa kutoa takwimu halisi ya kiasi cha mahindi kilichoharibika Kutokana na hali hii ameagiza Katibu Mkuu amsimamishe kazi Mtendaji mkuu wa mamlaka hiyo Bwana Charles Walwa na nafasi yake imechukuliwa na Bwana Deusdedt Mpazi ambaye atakaimu nafasi hiyo. Wengine waliosimammishwa kazi ni Mkurugenzi wa uendeshaji wa huduma Bi Anna Ngoo na Mkurugenzi wa Masoko Mikalu Mapunda na Meneja wa NFRA Songea Bwana Jeremia Mtafya.
Kuhusu zao la pamba Mhe. Waziri alieleza kwamba hadi sasa kuna wanunuzi 12 ambao wamepewa leseni ya kununua Pamba na pamoja na kuwa bei elekezi ya Pamba itakuwa ni Tsh 1000/= kwa kilo ya pamba mbegu, na hii ni baada ya majadiliano na wadau kutofikia muafaka Aliwashauri wakulima wawe wavumilivu wasiuze pamba yao chini ya hiyo bei elekezi. Wakati huo huo Mhe. Waziri aliagiza Halmashauri zinazopata fedha kutokana na mauzo ya pamba zisiwalazimishe wanunuzi kulipa hizo fedha kabla ya kununua kwa kulipa advance, na bodi ya pamba imeagizwa kusimamia hilo. Halamshauri zilishauriwa zisubiri hadi ununuzi ukamilike ndipo wadai fedha zao.
Wakati huo huo aliagiza Makao Makuu ya bodi ya pamba yahamishwe kutoka Dar es Salaam kwani Dsm hawalimi pamba na ihamie Mwanza na Vilevile bodi ya chai ihame kutoka DSM na iende Njombe ndani ya wiki mbili na bodi nyingine kama hizo zianze kujitayarisha kufanya hivyo.
Kuhusu Uvuvi katika bahari kuu Mhe. Waziri alieleza kwamba Tanzania ina eneo kubwa la kiuchumi katika bahari kuu lakini haina uwezo wa kuitumia na badala yake tumekuwa tukiwapa wenye uwezo kuvua kiasi wanachotaka kwa leseni ya dola za kimarekani 50,000 kwa muda wote wa leseni na kwa kuvua kiasi wanachotaka wao. Wavuvi hawa wanapovua samaki wa ziada huwa wanawatupa baharini au wanarudi kuja kutuuzia tena hapa sisi wenyewe kinyume na utaratibu.
Kutokana na hali hii Mhe. Waziri ameagiza masharti ya leseni yabadilishwe mara moja ili samaki wa ziada wawe wanaletwa hapa nchini. Aidha alishauri uangaliwe uwezekano wa kuvua kwa kushirikiana ili wanachopata tugawane wote.Kwa wale wote walio na leseni aliagiza waendelee kuzitumia hadi hapo zitakapokwisha na baada ya hapo leseni mpya zitolewe baada ya kubadilisha masharti . Mhe. Waziri aliendelea kueleza kwamba hivi sasa kuna meli takribani 105 ambazo zinavua katika bahari kuu na mamlaka ya Uvuvi katika bahari kuu wanajua hayo hivyo basi waagizwe walete samaki wa ziada hapa nchini.
Katika hatua za kuimarisha mamlaka ya Uvuvi katika bahari kuu Mhe. Waziri alimteua Bwana Hosea Gonza Mbilinyi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Uvuvi katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu kuanzia leo, Aidha aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo Bwana Rashid Hoza amerudishwa katika kituo chake cha kazi cha awali kuendelea na kazi zake.
Mhe. Waziri aliendelea kueleza kwamba Vilevile amebaini kwamba kuna matatizo ya uendeshaji katika vituo vya utafiti vya Uyole Mbeya na Naliendele Huko Mtwara hivyo basi Mkuu wa kituo cha Uyole Dr. Zacharia Malya anaondolewa na kuhamishiwa Katika kituo cha utafiti cha Seliani Arusha kuendelea na kazi zake za utafiti na Amemteua Dr Anold Msongi anayetoka katika kituo cha utafiti cha Ilonga kilichopo Kilosa Morogoro.
Katibu
mkuu wa wizara ya kilimo,mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) Dr.Yohana
Budeba aliyesimama mwenye koti jeusi akimkaribisha Mhe.Waziri wa
Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe Dr.Charles Tizeba aongee na waandishi wa
habari
|