Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt Mohammed Bahari mwenye suti akiongea na Meneja wa Kiwanda cha Bahari Food, alipowasili Kiwandani hapo |
Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt Mohammed Bahari mwenye suti akiwatambulisha Watumishi aliofatana nao katika Mkutano na Waandishi wa Habari |
Waandishi wa Habari na Baadhi ya Watumishi wa Wizara Waliohudhuria Mkutano wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na na Waandishi wa Habari Katika Kiwanda cha Samaki Bahari Food |
Baadhi ya Watumishi wa Wizara waliovalia Mavazi Maalum ya Kiwanda cha Kusindika Samaki kutoka kushoto Bi Mwanahamisi Msangi, Laila Kaduma na Bi Grace Pango kabla ya kutembelea ndani Kiwandani |
Bi Mwanahamisi Msangi Akitafakari kama atamudu kuvaa Kifunika Pua ili aingie kwenye Kiwanda cha Samaki |
Watumishi pamoja na Waandishi wa Habari wakielekea sehemu ya kwanza ya kupokelea Samaki |
Waandishi wa Habari Wakishangaa Uandaaji wa Samaki, Uhifadhi na Hatimaye Usafirishaji kwenda Nje ya Nchi |
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Uvuvi Bw Baraka Mghulwi Akifatilia Maelezo ya Meneja wa Kiwanda cha Samaki Hayupo Pichani |
Meneja wa Kiwanda cha Samaki Akitoa Maelezo kwa Wajumbe Walioshiriki Mkutano wa Wizara na Waandishi wa Habari katika Kiwanda cha Samaki Bahari Food. |
Waandishi wa Habari Wakionyeshwa Chumba Maalum cha Baridi kwa Ajili ya Kuhifadhi Samaki |
Mmoja wa Wafanyakazi akionyesha sehemu Wanayohifadhi Samaki baada ya kupokelewa kutoka Ziwani |
Katika Picha Huo Sio Urembo ni Nguo Maalum za Kuvaa ndani ya Kiwanda cha Samaki |
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Samaki cha Bahari Food wakiwa Kazini Wakati Waandishi wa Habari Walipotembelea Kiwanda hicho Kabla ya Mkutano kufanyika Kiwandani hapo. |
Sehemu ya kusafisha Samaki aina ya Pweza Wanaosafirishwa Nje ya Nchi Katika Picha Mfanyakazi akisafisha Pweza. |
Katika Picha Mfanyakazi wa Kiwanda cha Samaki Akionyesha Pweza Anayesafishwa, Kuhifadhiwa na BaadayeKuwekwa kwenye Boksi Maalum tayari kwa Kusafirishwa |
Mwakilishi kutoka Idara ya Habari Maelezo Bi. Fatma Salum akielezea kuhusu Mkutano huo ambao hufanyika kwa awamu |
Barafu inayozalishwa kwenye Kiwanda cha Samaki cha Bahari Food kwa ajili ya kuhifadhia Samaki Wasiharibike |
Mmoja wa Watumishi wa Kiwanda cha Bahari Food akitoa Maelezo kwa Waandishi wa Habari |
Sehem ya baridi sana wanapohifadhi Samaki kabla ya kupelekwa nje ya nchi |
Mwandishi wa Habari Akkishuhudia Chumba Maalum cha Kuhifadhi Hewa ya Baridi |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni