Nav bar

Ijumaa, 6 Machi 2015

MHE. KAMANI AKAMILISHA ZIARA NCHINI UFARANSA KWA KUTEMBELEA BANDARI YA UVUVI



Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani alipotembelea Bandari ya Uvuvi ya Boulogne (Port de Boulogne Sur Mer) ambayo ni ya tatu kwa ukubwa Barani Ulaya. Bandari ina eneo la Ha.150 ambalo lina huduma zote muhimu kwa Sekta ya uvuvi ikiwa ni pamoja na mnada wa samaki, viwanda vya kuchakata samaki, maabara ya kuhakiki ubora wa samaki, taasisi ya mafunzo na utafiti na mafunzo kwa wavuvi na wasindikaji samaki
Mhe. Dkt. Kamani akiwa katika mnada wa samaki na kupatiwa maelezo ya jinsi mnada wa samaki unavyoendeshwa.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akipata maelezo ya shughuli zinazofanywa na taasisi inayotoa mafunzo kwa wavuvi na wasindikaji wa samaki alipotembelea taasisi hiyo ambayo ipo katika Bandari ya Uvuvi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni