Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2025

SERIKALI YAENDELEA KUTOA MAFUNZO YA UPANDIKIZAJI VIFARANGA VYA SAMAKI KWENYE VIZIMBA NA MABWAWA

Picha
Na. Stanley Brayton, MWUV ◾ Vifaranga 1,500 vya pandikizwa Viwanja vya Maonesho Nanenane Dodoma. Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kutoa Mafunzo ya Upandikizaji Vifaranga vya Samaki ili kuwafanya wadau wa Sekta hiyo kuwa na Ujuzi wa kutosha katika kufuga Samaki pamoja na kuwasaidia kuwapa mbinu bora na ya kisasa ya ufugaji Samaki ili kuweza kujipatia kipato na lishe. Akizungumza katika zoezi hilo la Upandikizaji wa Vifaranga vya Samaki katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane ya Dkt. John Samwel Malecela, leo Oktoba 28, 2025 jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Nazael Madalla amesema lengo kubwa la kupandikiza Samaki katika Vizimba na Mabwawa yaliopo katika Viwanja vya Maonesho ya nanenane ni kuwawezesha wadau wa Sekta kupata Mafunzo ya teknolojia mpya ya ufugaji wa Samaki kwa njia ya Vizimba pamoja na Mabwawa. "Wizara inaendelea kuhamisha, kuendeleza pamoja na kusimamia shughuli za Ukuzaji Viumbe Maji kwa kut...

WAVUVI ZIWA NYASA WAKABIDHIWA MTAMBO WA KUKAUSHIA DAGAA NA SOKO LA KUUZIA SAMAKI

Picha
Na. Stanley Brayton, MWUV ◾ Wavuvi waahidiwa Vizimba vya kufugia Samaki. Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya Serikali ya elico Foundation imeikabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Soko la kuuzia Samaki na Mtambo wenye Thamani ya Milioni 129.98 kwa ajili ya kukaushia Dagaa ikiwa na uwezo uliosimikwa wa kukausha mazao hayo kwa wastani wa tani 3 hadi 5 kwa siku, mradi ambao umelenga kuongeza uzalishaji wa mazao hayo yenye kuathiriwa na changamoto ya hali ya tabia ya nchi ambao ulipelekea uchakataji wa zao hilo kuwa duni. Akizungumza katika Hafla ya Uzinduzi na Kukabidhi Mtambo huo, leo Oktoba 24, 2025, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede amesema Sekta ya Uvuvi imekuwa ikikabiliwa na upotevu mkubwa wa mazao ya uvuvi baada ya kuvunwa, hasa kwa dagaa ambao mara nyingi uharibika kutokana na kukaushia chini, na wakati mwingine mazao hayo hukutana na mchanga, matope, au mvua, na hivyo kupunguza ubora wake, bei yake sokon...

MEENA ATAKA USHIRIKIANO, TAASISI SITA ZA MIFUGO KUWA JENGO MOJA

Picha
Na. Edward Kondela Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena amezitaka taasisi sita kutoka sekta ya mifugo zinazojenga ofisi zake katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma, kusimamia ujenzi huo kwa ushirikiano ili ukamilike kwa wakati na viwango vinavyotarajiwa. Bi. Meena amebainisha hayo leo (21.10.2025) kwenye tukio la utiaji sahihi wa mkataba wa ujenzi wa jengo la ofisi za makao makuu ya taasisi hizo, zilizo chini ya wizara na kukabidhi eneo kwa mkandarasi wa ujenzi wa jengo hilo, ambapo amesema kukamilika kwa ujenzi kutasaidia kuondokana na tatizo la ukosefu wa ofisi bora kwa watumishi. Akizungumzia juu ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bodi ya Nyama Tanzania (TMB), Wakala ya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Wakala ya Maabara ya Mifugo Tanzania (TVLA) na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ambazo zitakuwa kwenye jengo moja, amesema anatambua TALIRI ndiyo imeingia makubaliano ya kimkataba lakini taasisi zingine tano zisijiwe...

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUBORESHA LISHE

Picha
Na. Martha Mbena, Dodoma.  Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa kitaifa na kimataifa kutekeleza mikakati inayolenga kuboresha sekta ya lishe kwa kuifanya kuwa na mifumo endelevu nchini. Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Dkt. Edwin Mhede wakati akifungua kikao cha kujadili  mradi wa Initiative on Climate Action and Nutrition (I-CAN) kilichofanyika  leo Oktoba 16, 2025 katika Hoteli ya Rafiki Jijini Dodoma.  Dkt.  Mhede amesema serikali inafanya kazi na wadau na mashirika mbalimbali kwa kufanya majadiliano ya  jinsi ya kuoanisha masuala ya kisera katika mabadiliko ya tabianchi na lishe bora. "Yaliyojadiliwa kwenye kikao cha leo yawe chachu ya kuifanya sekta hii ya lishe isogee mbele zaidi lakini mkakati wa mapitio ya sera kuhusu masuala ya lishe ni jambo la muhimu ", amesema Dkt. Mhede. Amesema wananchi wanategemea kupata afua za serikali zinazohimiza  matumizi ya ni...

SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI ZIMEENDELEA KUBORESHA LISHE NCHINI-MAJALIWA

Picha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa sekta za Mifugo na Uvuvi zimekuwa vinara kwenye mchango wa protini inayotokana na wanyama na samaki hapa nchini. Mhe. Majaliwa amesema hayo Oktoba 16,2025 wakati akifunga Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani kwenye Viwanja vya  Shule ya Sekondari Usagara mkoani Tanga ambapo amebainisha kuwa hatua hiyo imetokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali kwenye sekta hizo. “kwa sasa uzalishaji wa nyama umefikia taribani tani laki 6 na mayai takribani milioni 7 huku upande wa Uvuvi uzalishaji wa samaki umefikia hadi zaidi ya tani laki 5 hivyo nitoe rai kwa wananchi kuhakikisha tunaendelea kuhakikisha tunazalisha, tunahifadhi na kutumia vyakula vyenye virutubisho vingi na vyenye ubora wakati wote” Ameongeza Mhe. Majaliwa. Aidha Mhe. Majaliwa amewataka wananchi hususani wale wanaoishi vijijini kutumia Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani kufanya maamuzi sahihi kuhusu lishe bora inayohitaj...

WATUMISHI WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI WAPATIWA ELIMU YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Picha
Na. Fausta Njelekela, WMUV, Dodoma  Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamepewa elimu na huduma za upimaji wa Magonjwa yasiyoambukiza mahala pa kazi (NCDs) ikiwa ni sehemu ya kuzuia na kudhibiti magonjwa hayo. Zoezi hilo limefanyika Oktoba 15, 2025 katika ofisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma  ambapo wataalamu kutoka Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Chama cha Kisukari Tanzania (TDB) na Capital City Marathon walitoa huduma hiyo. Akizungumzia huduma na elimu hiyo Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mkurugenzi Msaidizi Utawala, Bw. Samwel Mwashambwa amesema zoezi hilo litaongeza uelewa na kuwahamasisha watumishi kujua umuhimu wa mtindo bora wa maisha na ufuatiliaji wa afya zao. Aidha, Bw. Mwashambwa amewashukuru wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Chama cha Kisukari Tanzania (TDB) na Capital City Marathon kwa kutoa elimu na upimaji wa magonjwa hayo yasiyoambukiza mahala pa kazi. Kwa upande wa...

SERIKALI YAHAMASISHA MATUMIZI YA MAYAI, MAZIWA TANGA

Picha
◼️Ni kupitia Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yanayoendelea mkoani Tanga Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wake wa Tasnia ya Maziwa na Kuku imeendesha kampeni ya kuhamasisha ulaji wa mayai na unywaji wa maziwa kupitia zoezi la ugawaji wa mazao hayo ya Mifugo kwenye shule za watoto wenye mahitaji maalum lililofanyika Oktoba 13,2025 jijini Tanga. Akizungumza wakati wa uendeshaji kampeni hiyo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary Yongolo amebainisha kuwa hatua hiyo inalenga kuinua kiwango cha ulaji wa mazao hayo kwa kujenga utamaduni wa matumizi yake kwa watoto hususan wanafunzi ili kujenga nguvu kazi ya Taifa itakayokuwa imara na yenye afya. “Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu inasema Tuungane pamoja kupata lishe bora kwa maisha ya sasa na ya baadaye na maisha ya baadae yanaanza utotoni kwa makundi haya madogo tuliyokuja kuyatembelea hapa” Ameongeza Bi. Yongolo. Akizungumzia umuhimu wa mayai na maziwa kwa wanafunzi, Afisa Lishe wa...

SERIKALI, WADAU KUJA NA MPANGO MKAKATI WA UJUMUISHWAJI BIOANUWAI KATIKA UVUVI

Picha
Na Hamisi Hussein - Dar es Salaam. Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetoa rai kwa washirika wa maendeleo ya uvuvi wa kitaifa na kimataifa kuwa mabalozi wa mabadiliko katika jamii wanazotoka  kwa kuendeleza ushirikiano wa kukuza uchumi wa buluu wa Tanzania kupitia ujumuishwaji wa masuala ya bioanuwai katika uvuvi.  Akifunga warsha ya ujumuishaji Masuala ya Bioanuwai katika Usimamizi wa Uvuvi Oktoba 8, 2025 katika Hoteli ya Giraffe Jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Dk. Charles Mhina amesisitiza umuhimu wa kujenga uelewa wa pamoja  wa kuoanisha uhifadhi wa bioanuwai na vipaumbele vya kitaifa, hasa katika nyanja za usalama wa chakula, maendeleo ya kiuchumi, na ustawi wa jamii. Dkt. Mhina amefafanua kwamba mafanikio ya muda mrefu ya sekta ya uvuvi yanategemea uhifadhi wa mazingira ya majini na hivyo  ni vema masuala yote yaliyomo katika Mfumo wa Kimataifa wa Kunming–Montreal wa Bioanuwai pamoja na Mkakati ...

WADAU WAHIMIZWA UMOJA UTUNZAJI RASILIMALI ZA UVUVI

Picha
 Ikiwa ni siku ya pili ya warsha ya kujadili ujumuishwaji wa masuala ya bioanuwai katika usimamizi wa rasilimali za uvuvi wadau wa maendeleo ya sekta ya uvuvi wamehimizwa kuwa na nguvu za pamoja zitakazosaidia kulinda na kutunza rasilimali za bahari na vyanzo vingine vya maji kwa ajili ya shughuli za uvuvi. Hayo yameelezwa Oktoba 8, 2025 katika Hoteli ya Giraffe Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina ambapo amesema serikali na wadau wengine wa maendeleo waweke  jitihada za pamoja katika utunzaji wa  mazingira ya viumbe maji itasaidia kuwa na uvuvi endelevu na kuinua uchumi wa jamii. Amehimiza washiriki wa warsha hiyo kutumia jukwaa hilo ili kubadilisha mtazamo kuhusu utunzaji wa mazingira ya bahari, vyanzo vya maji na rasilimali za uvuvi ili jamiii iweze kunufaika na sekta ya uvuvi  endelevu na kuondokana na umaskini. Aidha, Katika siku ya pili ya warsha hiyo majadiliano mbalimbali yamefany...

BI. MEENA AFUNGUA WARSHA YA UJUMUISHAJI BIOANUWAI KATIKA USIMAMIZI WA UVUVI

Picha
Na Hamisi Hussein - Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena amefungua warsha ya ujumuishaji wa masuala ya bioanuwai katika usimamizi wa uvuvi nchini iliyowakutanisha takribani washiriki 50 katika Hoteli ya Giraffe Jijini Dar es Salaam wakiwemo watafiti, wawakilishi wa halmashauri za wilaya, wataalam wa uvuvi wa ndani na wa kimataifa, asasi za kiraia, wawakilishi wa wavuvi wadogo na wadau wa maendeleo. Akifungua warsha hiyo leo Oktoba 7, 2025, Bi. Meena amewahimiza washiriki hao kuzitambua changamoto zinazoikabili mifumo ya Bioanuwai ili kulinda rasilimali za uvuvi nchini. "Ndugu washiriki tunapojadili ujumuishaji wa bioanuwai katika usimamizi wa uvuvi, ni muhimu kutambua changamoto zinazoikabili mifumo ya ikolojia nchini ukiwemo uvuvi  haramu ambao umesababisha kupungua kwa samaki  na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa yakibadilisha makazi ya viumbe na kuvuruga mifumo ya uzalishaji wa samaki  mambo haya  yanatishia bioanuwai na ust...

TANZANIA YA TATU AFRIKA MPANGO RASMI WA KUDHIBITI KICHAA CHA MBWA

Picha
Na Chiku Makwai: WMU Serikali kwa kushirikiana na wadau wa afya ya wanyama imeandaa  Mpango  Rasmi wa kutokomeza Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa ikiwa ni moja ya mkakati wa kufikia azma ya Dunia ya kuondokana kabisa na ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030. Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi Agnes Meena katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kichaa cha Mbwa Kitaifa yaliyofanyika leo Septemba 29, 2025 Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara. Bi. Meena amesema kwamba mpango huo ambao umeshapitiwa na kuridhiwa na Shirika la Afya ya Wanyama duniani (WOAH) utaratibu wa uchanji wa mbwa na paka wote nchini kwa muda wa miaka mitano. “Kupitia mpango huo, ni imani yetu kwamba hadi kufikia mwaka 2030 Tanzania itakua ni miongoni mwa nchi zitakazokuwa zimeutokomeza ugonjwa huu wa Kichaa cha Mbwa”,amesema Bi Meena. Aidha, ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa wataalam wa mifugo walio karibu yao au serikali ya mtaa ya eneo husika endapo watakutana na mnyama au mfugo wenye ...