SERIKALI KUIMARISHA MIKAKATI YA KUKUZA SHUGHULI ZA UKUZAJI VIUMBE MAJI ZIWA TANGANYIKA
Na. Stanley Brayton Serikali imeendelea kufanya juhudi za kuimarisha na kuweka mikakati bora ya kukuza shughuli za Ukuzaji Viumbe maji kupitia vizimba vya kufugia samaki ambapo njia hii inalenga kuboresha zaidi Uzalishaji wa Samaki na kukuza shughuli za uchumi kwa wananchi na kufungua fursa za uchumi. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, leo Januari 22, 2025 mkoani Dodoma katika Mkutano wa kujadili ni namna gani ya kuimarisha Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji kwa njia ya Vizimba na mashirikiano baina ya Wizara na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira "The Nature Conservancy" pamoja na Taasisi zingine, Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Nazael Madalla amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alielekeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha inahamasisha na kuendelea Ufugaji Samaki kwa njia ya Vizimba katika maeneno yote yanayofaa kiufugaji. "hapa nchini kwetu Ziwa Tanganyika ni moja ya maeneo ambayo ku...