Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2024

PROF. SHEMDOE AZINDUA BWENI LA WASICHANA CHUO LA LITA MOROGORO

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amezindua bweni la wanafunzi wa kike katika chuo cha Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) kampasi ya Morogoro lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 216 lililogharimu zaidi ya shilingi milioni 970 fedha za mapato ya ndani Akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo Aprili 06,2024,   Prof Shemdoe ameipongeza LITA kwa kufanikisha ujenzi huo kwa kutumia fedha za ndani ambapo kukamilika kwakwe kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na changamoto ya mabweni kwa wanafunzi katika kampasi hiyo Prof. Shemdoe alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendela kufanya jitihada za makusudi katika kuboresha miundombinu katika kampasi zote nane za LITA ambazo kwa sasa kila kampasi inaendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali pamoja na ukarabati wa majengo chakavu “Bajeti ya mwaka 2024/2025 imezingatia sehemu ya vipaumbele muhimu vinavyolenga kutatua changamoto zilizopo kwa awamu ili kuiwezesha Wakala kuwa na uwezo wa kudahi...