Wafugaji wa samaki Kanda ya Magharibu wamehimizwa kukitumia Kituo cha Mwamapuli kwa ajili ya kupata elimu ya ufugaji wa kisasa na kibiashara.
Hayo
yamesemwa leo (07.08.2023) na Wilbard Mapindo ambaye ni Afisa Uvuvi Msaidizi
kutoka Kituo cha Ukuzaji Viumbe Maji Mwamapuli kilichopo Wilayani Igunga mkoa
wa Tabora. Mapindo amesema kituo hicho kinafanya kazi kubwa ya utoaji elimu kwa
wafugaji wa samaki wa Kanda ya Magharibi na hata Kanda nyingine za jirani.
Wafugaji
wa samaki wamekuwa wakienda kutembelea kituoni hapo kwa lengo la kupata elimu
ya ufugaji bora wa samaki ambapo pia wamekuwa wakitakuliwa changamoto
mbalimbali ambazo wamekuwa wakikutana nazo katika shughuli ya ufugaji
wanayoifanya.
Pia
amesema kwa sasa kituo kimezidi kuimarika ambapo uzalishaji wa vifaranga vya
samaki umeongezeka hivyo amewatoa hofu wafugaji wa samaki kuwa wafike kituoni
hapo kwa ajili ya kununua vifaranga ambavyo bei yake pia ni Rafiki kwa mtu
yeyote.
Vilevile
Mapindo amewashi wafugaji wa samaki kuhakikisha wanawatumia Maafisa Ugani
waliopo katika maeneo yao kwa ajili ya kupata msaada wa kitaalam pale
wanapokutana na changamoto yoyote kwenye ufugaji.
Naye
Mussa Budaga ambaye ni mmoja wa wafugaji wa samaki kutoka Wilaya ya Kaliua
mkoani Tabora amesema kuwa wananufaika sana na uwepo wa Kituo hicho cha
Mwamapuli kwa kuwa kinawasaidia kupata elimu ya ufugaji bora wa samaki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni