Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Emmanuela Mawoko, (waliosimama wapili kushoto) akichangia mada kwenye Warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania, kuhusu Uongozi na Ufanisi wa mtandao katika jamii, (01.06.2023) Morogoro.
Mmoja wa washiriki wa Warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania, akichangia mada kwenye Warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, (01.06.2023).
Mhasibu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Bertha Shija akiwasilisha mada kuhusu Usimamizi wa Fedha katika biashara, kwa washiriki wa Warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania, katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro. (01.06.2023.)
Washiriki wa Warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania (TAWFA) wakionyesha Igizo kuhusu jinsi ya kuanzisha vikundi na kufikia malengo, Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, (01.06.2023).
Wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania (TAWFA) wa mikoa yote wakiwa kwenye makundi wakifanya majadiliano ya kazi waliyopewa na Mwezeshaji kutoka EASUN- Centre for Organizational Learning kuhusu kujenga uwezo wa kujitambua kwa kutumia dhana ya mikao, kwenye Warsha ya mafunzo yanayoendelea ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wa TAWFA. Morogoro, (01.06.2023)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni