Mkurugenzi Msaidizi Utumishi na Rasilimali Watu kutoka (WMUV), Bi. Mary Mwangiza akifundisha namna ya kutatua migogoro ndani ya Vikundi, kwenye Warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania, katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro. (02.06.2023)
Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi Emanuela Mawoko akiwasilisha mada ya taratibu za kupata leseni za kisafirisha mazao ya Uvuvi, kwenye Warsha inayoendelea ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania, katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, (02.06.2023.)
Bi. Irene Kiteku anayejishughulisha na shughuli za uvuvi kutoka Geita, akisawasilisha kazi ya makundi kuhusiana na Uongozi, ambayo walipewa katika warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania, katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, (02.06.2023)
Mkurugenzi wa shirika la "Environmental Management and Economic Development Organization" (EMEDO) Bi. Edith Lukanga akiwasilisha mada kuhusu Ushawishi na Utetezi, kwenye warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania, katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro. (02.06.2023)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni