Nav bar

Jumamosi, 1 Aprili 2023

WAZIRI ULEGA AKUTANA NA VIONGOZI WA KAMPUNI YA KUZALISHA CHANJO YA HESTER

 

Katibu wa Kamati ya Ushauri ya Uvuvi wa Kanda ya Ziwa Victoria, Bw. Kasiri Mayalu akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (hayupo pichani) wakati wa kikao baina yao na Waziri huyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ulipo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika jengo la NBC jijini Dodoma Machi 22, 2023.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kampuni ya kuzalisha Chanjo ya Hester muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo nao ofisini kwake jijini Dodoma Machi 22, 2023. Wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hester Africa, Bw. Raj Gera Kumar. Kulia ni Mkurugenzi wa Operesheni, Kiwanda cha Kutengeneza Chanjo cha Hester kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Wataalam kutoka Wizarani.


Mtendaji Mkuu wa Shirika la Wavuvi wa Ziwa Victoria (LVFO), Bw. Shigella Mahongo (kulia) akimueleza jambo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) alipofika ofisini kwa Waziri huyo jijini Dodoma Machi 22, 2023. Mahongo alikutana na Waziri huyo kwa lengo la kujitambulisha na kueleza mipango mbalimbali ya shirika hilo.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akimsikiliza Kiongozi wa Shirika la ITARE Financial Advisory ya Italia, Bw. Giorgia Traietti (kushoto) wakati alipokutana nae ofisini kwake jijini Dodoma Machi 22, 2023. Bw. Traietti alifika ofisini kwa Waziri huyo kujitambulisha na kuzungumzia kuhusu mpango wa biashara na mkakati wake unaokusudia kuanzisha kituo cha kunenepesha mifugo na kuchakata maziwa hapa nchini.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. David Silinde akiongea na Mkurugenzi wa Kanda, Shirika linaloshughulika na ulinzi na ustawi wa mnyama Punda la Brooke East Africa, Dkt. Raphael Kinoti (kushoto) alipokutana nae ofisini kwake jijini Dodoma Machi 22,2023.  Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha Society for the Protection of Animals (ASPA), Livingstone Masija. Viongozi hao walimtembelea Naibu Waziri huyo kwa lengo la kujitambulisha na kumueleza kwa ufupi majukumu ya Taasisi zao.


Mkurugenzi wa Kanda, Shirika linaloshughulika na ulinzi na ustawi wa mnyama Punda la Brooke East Africa, Dkt. Raphael Kinoti (wa pili kutoka kulia) akiongea na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri huyo jijini Dodoma Machi 22, 2023. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha Society for the Protection of Animals (ASPA), Livingstone Masija.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni