Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imepokea na kuridhia taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Kamati hiyo ilipokea na kuridhia taarifa hiyo katika kikao cha kupokea na kujadili taarifa ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika jijini Dodoma Machi 27, 2023.
Taarifa hiyo ya makadirio ya bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, jumla ni Shilingi Bilioni 292.5, ambapo sekta ya Mifugo fungu 99 ni Shilingi Bilioni 112.1 na Sekta ya Uvuvi fungu 64 ni Shilingi Bilioni 180.5.
Matumizi ya jumla ya fedha hizo ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi mengine ya kawaida.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. David Kihenzile akiongea wakati wa kufunga kikao cha Kamati cha kupokea na kujadili taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika jijini Dodoma Machi 27, 2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizoibuliwa na Wajumbe wakati wa kikao cha Kamati cha kupokea na kujadili taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika jijini Dodoma Machi 27, 2023.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati cha kupokea na kujadili taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika jijini Dodoma Machi 27, 2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (wa pili kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. David Silinde (wa kwanza kushoto) wakimuonesha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. David Kihenzile (katikati) baadhi ya vifungu vilivyomo katika taarifa ya makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka 2023/2024 iliyowasilishwa kwa Kamati hiyo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma Machi 27, 2023.
Sehemu ya Wataalam kutoka Wizarani wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa wakati wa kikao cha Kamati cha kupokea na kujadili taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika jijini Dodoma Machi 27, 2023.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Prof. Patrick Ndekidemi (katikati) akichangia hoja wakati wa kikao cha Kamati cha kupokea na kujadili taarifa ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika jijini Dodoma Machi 27, 2023.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni