Mkurugenzi Msaidizi Uendelezaji na Usimamizi wa Maeneo ya Malisho, Bw. Gabriel Bura (kushoto) akitoa maelezo ya namna ya uvunaji na uhifadhi wa malisho ya mifugo kwa baadhi ya wanakikundi wa kikundi cha uoteshaji nyasi za mifugo katika kijiji cha Msungua kata ya Sepuka wilayani Ikungi mkoani Singida ambapo amewasihi kulima malisho na kuyahifadhi ili yawasaidie kipindi cha kiangazi. (03.01.2023)
Mkurugenzi Msaidizi Uendelezaji na Usimamizi wa Maeneo ya Malisho, Bw.
Gabriel Bura (kulia) akiwaonesha baadhi ya wanakikundi wa kikundi cha uoteshaji
nyasi za mifugo katika kijiji cha Msungua kata ya Sepuka wilayani Ikungi mkoani
Singida namna ya kuchora mstari kwa ajili ya kuandaa sehemu ya kupanda mbegu za
malisho ya mifugo. (03.01.2023)
Afisa Mifugo Mkuu, Bw. Israel Kilonzo akiwaeleza wanakikundi wa kikundi cha uoteshaji nyasi za mifugo katika kijiji cha Msungua wilayani Ikungi mkoani Singida kuhusu aina za mbegu za malisho zilizopelekwa na mambo ya kuzingatia wakati wa kupanda. (03.01.2023)
Afisa Mifugo, Bw. Emmanuel Kato akiwaonesha wanakikundi wa
kikundi cha uoteshaji nyasi za mifugo katika kijiji cha Msungua wilayani Ikungi
mkoani Singida namna ya upandaji malisho aina ya Cenchrus. (03.01.2023)
Afisa Mifugo, Bw. Emmanuel Kato (kulia) akielezea namna ambavyo mbegu za malisho aina ya Cenchrus zinavyotakiwa kuchanganywa na udongo kabla ya kwenda kupandwa. (03.01.2023)
Mkurugenzi Msaidizi Uendelezaji na Usimamizi wa Maeneo ya Malisho, Bw. Gabriel Bura (kulia) akiwaonesha wanakikundi wa kikundi cha uoteshaji nyasi za mifugo katika kijiji cha Msungua kata ya Sepuka wilayani Ikungi mkoani Singida namna ya kufukia mbegu za malisho kwa kutumia udongo kidogo ili majani hayo yaweze kuota. Kushoto ni Afisa Mifugo Mkuu, Bw. Israel Kilonzo. (03.01.2023)
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Msaidizi Uendelezaji na Usimamizi wa Maeneo ya Malisho, Bw. Gabriel Bura (wa tatu kutoka kulia), Wataalam kutoka Sekta ya Mifugo, Halmashauri na Wanakikundi wa kikundi cha uoteshaji nyasi za mifugo katika kijiji cha Msungua wilayani Ikungi mkoani Singida wakati wa kukabidhi mbegu za malisho ya mifugo. (03.01.2023)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni