Nav bar

Jumatano, 16 Novemba 2022

WAZIRI NDAKI AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE, BW. JOSEPH BUTIKU

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki (kulia) akimsikiliza  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Bw.Joseph Butiku akizungumza mara baada ya kumtembelea waziri huyo ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma na kumpongeza kwa kazi anazozifanya.  (03.11.2022.)


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega (Mb), (wapili kutoka kulia) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Bw. Joseph Butiku (wa pili kutoka kushoto) baada ya Mkurugenzi huyo kumtembelea Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Mashimba Ndaki na Naibu Wake. Tukio hilo limefanyika makao makuu ya Wizara hiyo iliyopo  mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma. (03.11.2022)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Mashimba Ndaki(kulia) akimkabidhi  vitabu vya mipango mikakati ya maendeleo ya sekta ya Uvuvi na Mifugo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere  Bw. Joseph Butiku mara baada ya ugeni wake kwa Mhe. Ndaki. Tukio hilo limefanyika ofisini kwa waziri huyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma (03.11.2022)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni