Nav bar

Jumatano, 16 Novemba 2022

WATAALAM WA SEKTA YA MIFUGO WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAKUTANA


 Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Mifugo) Bw. Venance Ntiyalundura akizungumza wakati wa kikao cha siku mbili kinachowakutanisha baadhi ya wataalamu (hawapo pichani) wa Sekta ya Mifugo kutoka wizara zinazosimamia sekta hiyo na taasisi zilizo chini yake za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo amesema vikao hivyo ni muhimu kuhakikisha mambo mbalimbali yanayojadiliwa kuhusu sekta hiyo yanafanyiwa utafiti wa kina na kuleta matokeo chanya. (03.11.2022)



Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Zanzibar (ZALIRI) Dkt. Talib Saleh Suleiman akifungua kikao cha siku mbili Mjini Unguja, kinachowakutanisha baadhi ya wataalamu (hawapo pichani) wa Sekta ya Mifugo kutoka wizara zinazosimamia sekta hiyo na taasisi zilizo chini yake za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikiwa ni muendelezo wa kuunganisha ushirikiano kwa serikali zote mbili kubadilishana ujuzi na utaalamu na namna ya kukuza sekta ya mifugo, ambapo amewataka wataalamu hao kuhakikisha wanasimamia vyema maamuzi ya vikao hivyo ili viwe na tija kwa wananchi. (03.11.2022)


Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Angelo Mwilawa akiwasilisha mada juu ya umuhimu wa utafiti wa malisho bora ya mifugo pamoja na tafiti ambazo zimeleta tija katika kuongeza ubora wa nyama na maziwa wakati wa kikao cha siku mbili kinachowakutanisha baadhi ya wataalamu (hawapo pichani) wa Sekta ya Mifugo kutoka wizara zinazosimamia sekta hiyo na taasisi zilizo chini yake za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. (03.11.2022)


Mkurugenzi Msaidizi wa Epidemiolojia na Magonjwa Yanayovuka Mipaka kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Michael Madege akiwasilisha mada juu ya namna ya kudhibiti magonjwa ya mifugo kwa kutumia chanjo pamoja na hatua mbalimbali ambazo zimefikiwa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), wakati wa kikao cha siku mbili kinachowakutanisha baadhi ya wataalamu (hawapo pichani) wa Sekta ya Mifugo kutoka wizara zinazosimamia sekta hiyo na taasisi zilizo chini yake za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. (03.11.2022)


Baadhi ya wataalamu wa Sekta ya Mifugo kutoka wizara zinazosimamia sekta hiyo na taasisi zilizo chini yake za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa kwenye kikao cha siku mbili Mjini Unguja kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano katika sekta hiyo, ambapo katika siku ya kwanza wamejadili mambo mbalimbali yakiwemo ya kubadilishana ujuzi na utaalamu. (03.11.2022)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni