Nav bar

Jumatano, 19 Oktoba 2022

PROFESA NONGA AFUNGA KIKAO CHA MAFUNZO REJEA YA UFUATILIAJI WA MAGONJWA YA MIFUGO

 


Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Hezron Nonga akiongea wakati akifungua kikao cha program ya mafunzo rejea ya ufuatiliaji wa magonjwa ya mifugo kinachofanyika kwa siku tatu jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 11-13, 2022. Washiriki wa program hiyo ya mafunzo ni maafisa mifugo kutoka ngazi ya Wizara, Halmashauri na Taasisi za Mafunzo. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la misaada la Kimarekani la USAID, Bi. Carrie Read na kushoto ni Mratibu wa program hiyo kutoka Shirika la Kilimo na Chakula Duniani(FAO), Dkt. Moses Ole Neselle.


Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Prof. Hezron Nonga (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa kikao cha program ya mafunzo rejea ya ufuatiliaji wa magonjwa ya mifugo muda mfupi baada ya kufungua rasmi kikao hicho kinachofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo Oktoba 11, 2022.


Sehemu ya Washiriki wa kikao cha program ya mafunzo rejea ya ufuatiliaji wa magonjwa ya mifugo wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa mbalimbali katika kikao hicho kinachofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku tatu kuanzia Oktoba 11-13, 2022. Program hiyo imeandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni