Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega ametembelea Maonyesho ya Uwekezaji na Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Stendi ya Zamani maili moja Mkoani Pwani.
Maonyesho haya yamezinduliwa Jana na Rais wa awamu ya nne wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete yakiwa na kauli
mbiu isemayo; Pwani ni sehemu sahihi kwa uwekezaji, pamoja tujenge Viwanda kwa
uchumi na ajira endelevu huku ikishirikisha kampuni, Mashirika na taasisi
mbalimbali.
Mhe.Ulega ameridhishwa na Mpango kabambe wa Halmashauri ya Mji
Kibaha wa kupanga, kupima na kutenga maeneo maalum ya uwekezaji wa Viwanda
kwenye Kata za Visiga, Mbwawa na Pangani kuwa utaratibu huo ni mzuri kwani
unarahisha upatikaji wa bidhaa lengwa
Awali alitembelea Banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi ambapo alipata utaratibu wa namna Wizara hiyo inavyorahisisha utoaji
wa hati kwa wawekezaji nchini.
Hata hivyo, ametoa rai kwa wataalam wa Wizara hiyo kuongeza Kasi
ya upimaji wa maeneo ili kupunguza Migogoro ya Ardhi ambayo imeshamiri hasa
Mkoa wa Pwani.
Mhe.Ulega ameridhishwa na pia na kiwanda cha Hester Bioscience Afrika limited kinachotengeneza chanjo za wanyama na kwamba kimekuwa Mkombozi kwa Serikali kwani badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi Sasa zinapatikana hapa nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni