Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa kuwasilishwa kwa mpango wa mabadiliko ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) katika viwanja vya bunge jijini Dodoma, ambapo Naibu Waziri Ulega amesema wizara itahakikisha NARCO inakuja na mabadiliko makubwa katika kukuza Sekta ya Mifugo nchini. (20.09.2022)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda, akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa kuwasilishwa kwa mpango wa mabadiliko ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) katika viwanja vya bunge jijini Dodoma, ambapo amesema wizara itahakikisha inawapima viongozi mbalimbali wa wizara katika kufikia matokeo chanya ya kuifanya NARCO kuwa ya kisasa zaidi. (20.09.2022)
Wakurugenzi kutoka idara mbalimbali za Sekta ya Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa kuwasilishwa kwa mpango wa mabadiliko ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) katika viwanja vya bunge jijini Dodoma. (20.09.2022)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni