Nav bar

Jumapili, 14 Agosti 2022

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA MAONESHO YA NANENANE AGOSTI 5, 2022

Dkt. Isaya Kibasa kutoka ZVC Mtwara akitoa mafunzo kwa wataalam wa Halmashauri juu namna ya utoaji vibali vya afya ya Mifugo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa MIMIS. Mafunzo hayo yamefanyika kwenye Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nanenane – Ngongo Mkoani Lindi. (05.08.2022)

Mkurugenzi wa BOT Kanda ya Kusini, Ndg. Nassor A. Omary (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Ukuzaji Viumbe Maji Baharini, Dkt. Hamisi Nikuli wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nanenane – Ngongo Mkoani Lindi. (04.08.2022)

Ndg. Zacharia Mchanga (kulia) kutoka Wakala ya Maabara za Veterinari Tanzania (TVLA) akionyesha aina mbalimbali za dawa za mifugo kwa wadau waliotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nanenane – Ngongo Mkoani Lindi. (05.08.2022)

Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti kutoka Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Bi. Eileen Nkondola (kushoto) akiwaelimisha wadau juu ya teknolojia ya ufugaji wa samaki kwa kutumia bwawa linalohamishika wakati walipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nanenane – Ngongo Mkoani Lindi. (05.08.2022)

Madaktari wa Mifugo kutoka Baraza la Veterinari Tanzania, Dkt. Caroline Uronu(wa kwanza kulia) na Dkt. Winstone Bill, wakitoa elimu kwa wadau wa Mifugo jinsi ya kuomba vibali kwenye mfumo wa "MIMIS" vinavyotelewa na baraza hilo walipoenda kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maonesho ya Wakulima nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea mkoani Morogoro Agosti 05,2022.


Afisa Uvuvi Mkuu, kutoka Maabara ya Taifa ya Uvuvi, kanda ya Mashariki na Pwani, Longinus Tegulirwa, akitoa maelezo  jinsi maabara hiyo inavyofanya kazi ya kuhakikisha ubora wa Samaki na mazao yake kabla ya kufika kwa mlaji kwa mdau alipoenda kutembelea  kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya wakulima nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea kufanyika Morogoro, Agosti 5,2022.

Afisa Uvuvi kutoka kituo cha ukuzaji viumbe maji cha Kingolwira Mkoani Morogoro, Bi. Gilness Frank, akitoa maelezo kuhusu ufugaji bora na endelevu wa samaki aina ta Sato na Kambale, kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya wakulima nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea Mkoani Morogoro, Agosti 5,2022.

Afisa Uvuvi Mkuu, Bi. Mkomanile Mahundi (wa pili kushoto) akitoa elimu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha dar es salaam (UDSM) na  kuwaeleza malengo yaliyowekwa kwenye Sekta ya uvuvi ikiwa ni pamoja na kuzalisha vifaranga vya samaki visivyopungua milioni tano  walipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya nanenane kwenye kiwanja cha nyamhongolo Mkoani Mwanza, Agosti 05, 2022.

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Joachim Mkangaa (kushoto) akiwaelimisha wadau juu ya teknolojia ya ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba  wakati walipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nanenane – Nyamhongolo Mkoani Mwanza Agosti 05, 2022

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni