Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid
Tamatamah(Mgeni rasmi) akiongea wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Kupitia na
Kuthibitisha Mpango Kabambe wa Uvuvi unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma
kuanzia Disemba 20- 21, 2021.Ambapo aliwataka Washiriki wa Mkutano huo kutumia
fursa hiyo kupitia kwa makini kipengere kwa kipengere na hatimaye kuthibitisha
rasimu ya Mpango huo wa Mwaka 2021.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid
Tamatamah (kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,
Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), Prof. Yunus Mgaya muda mfupi baada ya
kufungua Mkutano wa Kupitia na Kuthibitisha Mpango Kabambe wa Uvuvi unaofanyika
kwa siku mbili jijini Dodoma kuanzia Disemba 20-21, 2021.
Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi, Bw. Magese Bulayi akitoa neno fupi
kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua Mkutano wa Kupitia na Kuthibitisha
Mpango Kabambe wa Uvuvi unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma kuanzia
Disemba 20-21, 2021.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid
Tamatamah (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Sekta ya
Uvuvi wanaoshiriki Mkutano wa Kupitia na Kuthibitisha Mpango Kabambe wa Uvuvi
unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma kuanzia Disemba 20-21, 2021.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni