Nav bar

Jumanne, 13 Aprili 2021

WACHUNAJI WA NGOZI KATIKA JIJI LA DODOMA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU MBINU BORA ZA UCHUNAJI NGOZI NA MATUMIZI YA VIFAA STAHIKI.

 

Afisa Mifugo Mkuu (Idara ya Uzalishaji na Masoko) kutoka WMUV, Bi. Mariam Muchakila (kulia) akizungumza na wachunaji wa ngozi wa Jiji la Dodoma kuhusu mbinu bora za uchunaji ngozi na matumizi ya vifaa stahiki wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika machinjio ya Dodoma yaliyopo eneo la Kizota. (12.04.2021)
Mtaalam wa Ngozi ambaye pia ni Afisa Mstaafu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Emmanuel Muyinga (kulia) akitoa mafunzo kwa wachunaji wa ngozi wa Jiji la Dodoma kuhusu mbinu bora za uchunaji ngozi na matumizi ya vifaa stahiki wakati  wa mafunzo yaliyofanyika katika machinjio ya Dodoma yaliyopo eneo la Kizota. (12.04.2021)
Afisa Masoko na Mahusiano kutoka Kiwanda cha Ngozi cha Kilimanjaro, Fredrik Njoka (kulia) akizungumza na wachunaji wa ngozi wa Jiji la Dodoma wakati wa mafunzo kuhusu mbinu bora za uchunaji ngozi na matumizi ya vifaa stahiki yaliyofanyika katika machinjio ya Dodoma yaliyopo eneo la Kizota. (12.04.2021)
Mkuu wa Kitengo cha Usafirishaji (Kiwanda cha Ngozi cha Kilimanjaro) Bw. Siyanremi Luggajo akikagua ngozi iliyotoka kuchunwa katika machinjio ya Dodoma ambapo ameridhika na ubora wa ngozi hizo kuwa zinafaa kwa matumizi ya kutengenezea bidhaa katika kiwanda chao. (12.04.2021)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni