Mhandisi kutoka Kampuni ya
ZECO, Emmanuel Rodrick (kushoto) akitoa maelezo kwa Mhandisi kutoka WMUV,
Masanga Makoje (mwenye flana ya njano) jinsi maji yaliyotokana na mvua kubwa,
yalivyobomoa ukingo uliokarabatiwa na hatua zitakazochukuliwa kurekebisha hali
hiyo ili maji yajae. Bwawa hilo lipo katika kijiji cha Narakauo, wilayani
Simanjiro, mkoani Manyara. (16.11.2020)
Mhandisi Masanga Makoje
(kulia) akiwa na Mhandisi wa Kampuni ya ZECO, Emmanuel Rodrick wakikagua
ukarabati wa bwawa la maji kwa ajili ya matumizi ya Mifugo na Binadamu katika
kijiji cha Narakauo, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara. (16.11.2020)
Mhandisi kutoka WMUV, Masanga
Makoje (mwenye flana ya njano kushoto) akitoa maelezo ya ushauri kwa Mhandisi
wa Kampuni ya ZECO, Emmanuel Rodrick kuhusu ukarabati wa bwawa la maji kwa
ajili ya matumizi ya Mifugo na Binadamu unaoendelea kufanyika katika bwawa hilo
kwenye kijiji cha Narakauo, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara. (16.11.2020)
Bwawa la maji kwa ajili ya
matumizi ya Mifugo na Binadamu ambalo linakarabatiwa baada ya udongo uliokuwa
unatumika kama kingo za kuzuia maji kusombwa kufuatia mvua kubwa iliyonyeesha
katika kijiji cha Narakauo, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara. (16.11.2020)
Picha ya pamoja ya viongozi
wa kijiji cha Narakauo, Mhandisi kutoka WMUV, Masanga Makoje (wa nne kutoka
kulia) na Mhandisi wa Kampuni ya ZECO, Emmanuel Rodrick (wa pili kutoka
kushoto) baada ya kufanya ukaguzi kwa pamoja kuona maendeleo ya ukarabati wa
bwawa la maji kwa ajili ya matumizi ya Mifugo na Binadamu katika kijiji cha
Narakauo, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara. (16.11.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni