Pichani ni Jengo jipya la
Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) linalojengwa Kunduchi, jijini
Dar es Salaam kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia mradi wa SWIOfish. Timu ya
Wataalam kutoka SWIOfish ilitembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya ujenzi huo
ambao unatarajiwa kukamilika hivi karibuni. (11.09.2020)
Mratibu wa Mradi wa SWIOfish,
Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga, Asha Churu akieleza jambo kwa Viongozi wa
Serikali ya Kijiji cha Zingibari na Viongozi wa BMU muda mfupi baada ya kufanya
ukaguzi wa ujenzi unaondelea wa Ofisi ya BMU kijijini hapo. Timu ya Wataalam
kutoka Mradi wa SWIOfish walitembelea Wilaya hiyo kufanya ufuatiliaji wa
maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo. (12.09.2020)
Mwenyekiti wa Kijiji cha
Zingibali, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga, Ibrahim Mahasham akitoa maelezo
kuhusu ujenzi wa Ofisi ya BMU ya kijiji cha Zingibari kwa Timu ya Wataalam
kutoka Mradi wa SWIOfish waliokwenda kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya
utekelezaji wa mradi Wilayani humo. Ujenzi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia
kupitia Mradi wa SWIOfish. (12.09.2020)
Timu ya Wataalam kutoka Mradi
wa SWIOfish wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha
Zingibari na Viongozi wa BMU, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga walipotembelea
kijiji hicho kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa SWIOfish. Katikati
ni Afisa Mawasiliano, Mradi wa SWIOfish, Amina Kiaratu. Wa tatu kutoka kushoto
ni Afisa Ufuatiliaji na Utathimini, Mradi wa SWIOfish, Furaha Kabuje na wa kwanza
kulia ni Mratibu wa Mradi wa SWIOfish, Wilayani Mkinga, Asha Churu. (12.09.2020)
Mwenyekiti wa Kamati ya
Takwimu ya BMU, Kijiji cha Kaole, Wilayani Bagamoyo, Salum Iddy (Kulia) akifafanua
jambo kwa Timu ya Wataalam kutoka Mradi wa SWIOfish waliotembelea Wilaya ya
Bagamoyo kufanya ufuatiliaji wa mafanikio ya utekelezaji wa Mradi wa SWIOfish.
Wa pili kulia ni Afisa Ufuatiliaji na Utathimini kutoka Mradi wa SWIOfish,
Furaha Kabuje. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mawasiliano wa Mradi wa SWIOfish,
Amina Kiaratu. Wengine ni Viongozi wa BMU ya Kaole, Wilayani Bagamoyo.
(11.09.2020)
Ujenzi wa Ofisi ya BMU ya
Kijiji cha Zingibari, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga ukiwa katika hatua ya
msingi kama inavyoonekana katika picha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni